Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mambo vipi ustadh,..umekula futari pekeyako?
Niamekuandalia Daku
FB_IMG_1617232207345.jpg
 
Kuna siku nilikuambia kama sikosei, M/kwerekwe pale karibu na Kivulini kwa wauza mitumba au karibu na Fuoni pr sc.
woyoooooo kivulini, lile eneo kwa sasa limetolewa milango ya duka.
pamechangamka kuliko zamani.
===========
zamani tulikuwa tunapaita BAM, palikuwa na ukumbi ulikuwa unaonyeshwa mpira wa miguu.
 
kwetu sisi Ijumaa mambo huwa hivi
===============

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla alisema Fadhila za utukufu wa Mwezi wa Ramadhani zinaeleweka na Waumini waliowengi na kinachohitaji kwao kuendeleza Ibada hata baada ya kumalizika kwa Mwezi huo.
Akizungumza na Waumini wa Dini ya Kiislamu mara baada ya kukamilika kwa Ibada ya Sala ya Ijuma kwenye Msikiti Jeshi Jang’ombe Mheshimiwa Hemed Suleiman alieleza kwamba mshikano
 
Alisema wapo baadhi ya Waumini wamekuwa na tabia ya kufanya Ibada kwenye Mwezi wa Ramadhan pekee jambo ambalo linakwenda kinyume na ucha mungu unaopaswa kutekelezwa muda wote wa maisha ya Muumini.
Mheshimiwa hemed aliendelea kuwakumbusha waumini hao kuwa, mwezi wa ramadhani ni kipindi cha kusaidiana, kwa kuzidisha utoaji wa sadaka na kuwaasa wenye tabia ya kurimbikiza vyakula hadi kuvimwaga, hali ya kuwa wapo wenzao, ambao hawana cha kukila.
 
Akigusia suala la bei za bidhaa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema serikali imekuwa ikisamehe ushuru kwa bidhaa za vyakula ili kuwasaidia wananchi kumudu futari, lakini inasikitisha kuona baadhi yao hupandisha bei za bidhaa jambo ambalo linawakwaza wananchi kupata huduma hiyo.

Aidha alitanabahisha kwamba baadhi ya Wafanyabiashara wanashindwa kuwa na uchungu Kwa Wananchi wanaowahudumia na badala yake wanaufanya mwezi Mtukufu wa Ramadhan kuwa ni chumo kubwa la kupata faida iliyonona tabia ambayo inastahiki kuondoshwa.
 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaomba Wananchi Mitaani pale wanapoona uzembe wa makusudi ni vyema wakatoa taarifa mapema katika ngazi iliyo karibu nayo na baadae itaifikisha katika ngazi husika.
Mapema akitoa Hotuba katika sala ya Ijumaa MaalimMashi Yussuf Mashi aliwakumbusha wale walioamini kuendelea kufunga Mwenzi Mtukufu wa Ramadhan na kinyume chake ni kuukataa Uislamu jambo ambalo dhambi isiyosameheka.
 
Maalim Mashi Yussuf aliwaeleza Waumini hao kwamba lazima wazingatie taratibu za Ibada katika kujiepusha na vitimbi vya Shetani kwa kusoma sana Kitabu Kitakatifu cha Quran ibada itayokwenda sambamba na kuzidisha sala za Usiku.
Alisema hatua hiyo ndio njia pekee kwa Kila Muumini atakayejikita kwa hayo atafanikiwa kumshinda shetani na tayari atajikaribisha kwa Muumba wake katika utekelezaji wake wa ucha Mungu.
==============
asiyemjua makamu wa pili ndiye huyo pichani
1618521899789.png
 
Nitaendeleza alipofikia Maalim Seif katika kuwasaidia Masheikh wa Uamsho - Mheshimiwa Othman Masoud
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, ameelezea utayari wake wa kufanya kila awezalo, akishirikiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, kuhakikisha kuwa Wazanzibari waliokamatwa na kupelekwa Tanzania Bara kushitakiwa kwa tuhuma za makosa yanayohusiana na ugaidi wanatendewa haki.
 
Akizungumza na waumini baada ya Sala ya Ijumaa kwenye Msikiti wa Maghfira uliopo mtaa wa Mchangani, Mjini Unguja, hivi leo, Mheshimiwa Othman amesema kwamba anaendeleza juhudi zilizoanzishwa na mtangulizi wake, Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad, katika kulipatia ufumbuzi suala hilo ambalo limekuwa likiwaumiza wananchi wengi wa Zanzibar, mbali ya wenyewe mahabusu hao na familia zao.
 
Wakati wa uhai wake, Maalim Seif alishirikiana vyema na Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi, na walichukuwa juhudi kubwa kuhakikisha kwamba suala la Masheikh wa Uamsho linapatiwa ufumbuzi. Na kwa kweli, juhudi zao zinaelekea kupata mafanikio. Nami nitaendelea kuungana na Rais Dkt. Mwinyi kuendeleza palipofikia". Alisema Makamu huyo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.
Mheshimiwa Othman ameongeza kwamba sifa za waja wema ni kusema ukweli na kutenda haki, ikiwa ni pamoja na kutimiza dhamana wanazokabidhiwa.
1618522010523.png
 
Kwangu ni amana na dhamana, maana nafasi hii ya Umakamu wa Kwanza wa Rais niliyonayo, nimeachiwa na mtangulizi wangu, Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad. Kwa hivyo, nina dhamana ya kuhakikisha yale aliyoyaanza yeye katika kuwasaidia ndugu zetu hawa Masheikh wa Uamsho kupata haki yao, na mimi niendeleze katika hilo". Alisisitiza kwa waumini hao.

Vile vile, Makamu huyo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amesema kuna haja kubwa ya kuwasaidia Masheikh wa Uamsho pamoja na familia zao, kwani ni muda mrefu sasa wapo mahabusu wakisubiri hatima ya kesi yao.
 
"Kipindi hiki cha Ramadhani tujitahidini kuwasaidia wenzetu wale ambao wana mahitaji. Na kwa mujibu wa sheria za nchi yetu, hakuna kosa kwa mtu kutoa msaada kwa Masheikh wale wa Uamsho au familia zao. Ni vyema sana kufanya hivyo kwa mwezi huu wa Ramadhani na hata baada, kwani katika jamii zetu wapo watu wengi wanaohitaji misaada kutoka kwetu", alinasihi makamu wa kwanza wa Rais

Sambamba na hilo, uongozi wa Masjid Maghfira umemuomba Makamu huyo wa Kwanza wa Rais kuwa mlezi wa msikiti huo, ombi ambalo Mheshimiwa Othman amelikubali.
1618522104962.png

===============

furniture za msikiti🙌🙌🙌🙌
 
Back
Top Bottom