Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

PSG itambakiza mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 34, kwa msimu mmoja zaidi lakini iko tayari kuruhusu mshambuliaji wa Brazil Neymar, 30, leave. (Sky Sports News)
 
Juventus iko kwenye mazungumzo ya kumsajili winga wa Argentina Angel di Maria, 34 kwa uhamisho huru mwishoni mwa msimu baada ya kuamua kutoongeza mkataba wake. (Goal)
 
West Ham itaanzisha mazungumzo na Hull City kwa ajili ya kumsajili mshambiliaji muingereza Keane Lewis-Potter.
 
Stade Reims itamruhusu mshambuliaji mfaransa mwenye miaka 19 Hugo Ekitike kuondoka klabuni hapi kwa ada ya £30m msimu wa kiangazi na Newcastle wanatarajia kurejesha nia yao ya kumsajili baada ya kufanya mazungumzo na kinda huyo mwezi Januari. (Shields Gazette)
 
Ilkay Gundogan, 31, anasema angefurahi kumaliza soka lake Manchester City, lakini kiungo huyo wa Ujerumani angetamani kutimkia ligi ya Uturuki Turkish au MLS ya Marekani mkataba wake utakapomalizika mwaka 2023. (Sport 1, in German)
 
Neco Williams anasema hajua atacheza klabu gani msimu ujao. Mlinzi huyo wa kulia wa Wales mwenye miaka 21 kwa sasa anacheza kwa mkopo Fulham akitokea Liverpool. (Wales Online)
 
Chelsea huenda ikafufua tena mbio zake za kumnasa mlinzi wa Sevilla na Ufaransa Jules Kounde, 23, dirisha lijalo baada ya kuthibitishwa kuwa Antonio Rudiger ataondoka klabuni hapo. (Football London)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…