Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,970
- 1,252,247
Kama maisha yamekupa nafasi ya upendeleo basi usianze kuwaita wengine wavivu
Sawasawa 🤣
Kumbukumbu muhimu
SawaMaisha yana tabia ya kukurudishia kile kile unachotoa. Ukiwa mtu wa hasira utakutana na watakaokukasirisha. Ukiwa mtu wa amani, maisha yanakukutanisha na watakaokupa amani.
✔️✔️Maisha ni safari ya kila mmoja kwa wakati wake, usiruhusu presha ya watu ikutoe kwenye njia yako, maana kila mtu ana muda wake wa kung'aa na kufikia hatima yake
✔️✔️Maisha ni safari ya kila mmoja kwa wakati wake, usiruhusu presha ya watu ikutoe kwenye njia yako, maana kila mtu ana muda wake wa kung'aa na kufikia hatima yake
✔️✔️✔️Ni bora kuanza safari mpya ambayo una uhakika na unapokwenda kuliko kufuata njia usiyojua unapokwenda
✔️✔️✔️Maisha ni Mtazamo
Kuna Wakati unaweza kuona kwanini huendelei kumbe umefungwa Mtazamo wako kwa mambo yanayokufanya ubaki vile vile siku zote.
Ukweli huuUkiwa mtu wa majungu, dharau na kushushua watu, utakutana na hao hao watakaokupiga majungu, watakaokushushua na kukudharau. Ukiwa mtu wa kuheshimu utu wa watu na kustahi faragha zao, maisha yanakurudishia heshima na staha. Unapata kile kile unachowatendea wengine —na kuzidishiwa
✅️Mkumbushe mwanao kuwa maisha ni safari ya kipekee kwa kila mmoja, na kile kinachokuwa bora kwake, hakiwezi kuwa bora kwa mwingine. Kila mtu ana malengo, changamoto, na njia yake ya kufikia mafanikio
✅️✅️Maisha ni safari ndefu inayohitaji upendo, amani na uvumilivu, tusichoke kupambana ipo siku mambo yatakaa sawa tu.