myoyambendi
JF-Expert Member
- Sep 13, 2013
- 174,811
- 721,144
Asubuhi njema mamalishe wote, Asubuhi ya chai na supu
👍👍Hamna kitu kizuri kama ukiaa sehemu watu wakaongelea wema wa mtu wako wa karibu na siyo madhaifu yake. Hakuna binadamu aliye mkamilifu ila tujenge tabia ya kuongelea watu vyema hususani wale ambao wamekua watu wema kwenye maisha yetu.
✅️✅️✅️Urafiki ni kitu cha thamani kubwa sana. Ukiwa na marafiki wa kweli unakuwa na manufaa mengi ikiwemo ushauri wa kimaendeleo ili kuendana nao. Unapokuwa na shida au raha marafiki ni watu wa kwanza kuwa na wewe. Hata hivyo ili kudumisha urafiki kunahitaji uvumilivu na gharama pia.
👍👍Katika maisha hakuna rafiki mzuri na wakweli kama muda, Mtu akikupenda mpe muda, akikuchukia mpe muda. Mtu akiona wewe hufai na hauna maana mpe muda, mtu akikuacha katika magumu mpe muda Hata yule asiyekupa muda mpe muda. Muda ndiye jawabu la mambo mengi sana
Urafiki mzuri, ujirani mwema, mahusiano yenye afya ni zao la malezi bora lakini malezi bora hutoka kwa baba na mama wanao pendana kwanza wao
Sifa kuu ya Urafiki mwema ni maelewano ya dhati na kushibana
✔️✔️✔️Siku za nyuma kidogo, ukimkopa mtu kitu au pesa ilikuwa heshima kubwa na pia njia ya kuongeza au kudumisha urafiki na ujirani mwema,..Ila siku hizi ukimkopa mtu , jua tiyari umeshaingia uhasama hasa wakati unafatilia madai yako, usipokuwa makini hata uhai unaweza poteza.
👍👍Siku za nyuma kidogo, ukimkopa mtu kitu au pesa ilikuwa heshima kubwa na pia njia ya kuongeza au kudumisha urafiki na ujirani mwema,..Ila siku hizi ukimkopa mtu , jua tiyari umeshaingia uhasama hasa wakati unafatilia madai yako, uspokuwa makini hata uhai unaweza poteza.
SawasawaKuwa rafiki mwema kwa kila mtu mwenye urafiki wa kweli kwako.
SahihiUsirithi Maadui, Usiwe Tayari Kumchukia Mtu Anayechukiwa na Rafiki Yako Ukidhani Ndo Urafiki Mwema.
📌📌📌Tujenge urafiki mwema kama wa Limao na Tangawizi ili tuweze kusaidiana na kutibiana pale inapobidi.Na tuache vinyongo vya kila mara ambavyo havina sababu.Vinyongo ni ugonjwa.Kumbuka ya kuwa njia ni nyembamba sana