myoyambendi
JF-Expert Member
- Sep 13, 2013
- 174,811
- 721,144
✅️✅️✅️Rafiki wa kweli ni yule mtu anayefahamu uliyopitia na unayopitia sasa na bado anaamini utafanikiwa hapo baadae.
✅️✅️✅️Rafiki wa kweli ni yule mtu anayefahamu uliyopitia na unayopitia sasa na bado anaamini utafanikiwa hapo baadae.
SahihiUkipata Matatizo Ndipo Utagundua Kuwa Huna Marafiki Wengi , Bali Una Watu Wengi Mnaofahamiana
✅️✅️✅️Ubinadamu kazi sana, Mtu anayekufahamu hataki ufanikiwe anahitaji asiye mfahamu ndio afanikiwe, Ila akipata shida Anaamini anaye mfahamu ndio anaweza Kumsaidia na sio yule Asiye mfahamu.
Ujumbe muhimuKamwe usikubali kuwa kwenye mahusiano unayohisi kama mapambano ya mara kwa mara. Unastahili mtu ambaye atakuwa mshirika wako, msaidizi wako. Kumbuka, mwenza wako anapaswa kuwa eneo lako salama, siyo chanzo kingine cha maumivu au msongo katika maisha yako. Unastahili bora zaidi.
Hakika kabisaUrafiki mwema ni maelewano ya dhati na kushibana
👍👍Mali sio rafiki wa kudumu, lakini rafiki ni rasilimali ya kudumu"Kuwa mkweli kwa rafiki yako, thamini sana utu wake na elewa ubinadamu wake. Urafiki mwema ni hazina kubwa, unaoweza kukufaa sana sana.
📌📌📌Sio kila Mtu Unayemuona ni Rafiki Anaweza Kuwa na Sifa na Vigezo vya Rafiki*Maana Urafiki MWEMA Hujidhihirisha kwa Jinsi Anavyoshirikiana na Wewe Kwenye Hali ya Matatizo Hivyo Basi Jifunze Kutofautisha Kati ya RAFIKIna JAMAA
Kamwe usikubali kuwa kwenye mahusiano unayohisi kama mapambano ya mara kwa mara. Unastahili mtu ambaye atakuwa mshirika wako, msaidizi wako. Kumbuka, mwenza wako anapaswa kuwa eneo lako salama, siyo chanzo kingine cha maumivu au msongo katika maisha yako. Unastahili bora zaidi.
Sio kila Mtu Unayemuona ni Rafiki Anaweza Kuwa na Sifa na Vigezo vya Rafiki*Maana Urafiki MWEMA Hujidhihirisha kwa Jinsi Anavyoshirikiana na Wewe Kwenye Hali ya Matatizo Hivyo Basi Jifunze Kutofautisha Kati ya RAFIKIna JAMAA
Ni jambo zuri sana kuwa na marafiki
Ila usifanye kosa la kuwathamini sana marafiki zako kuliko ndugu zako..
Ni rahisi sana urafiki kufa kuliko undugu
Maisha Ya Leo Ili Uonekane Una Upendo Kwa Ndugu Au Kwa Watu Wengine Basi Jitahidi Uwe Unatoa Hata Kile Kidogo Ulichonacho Hapo Utaonekana Una Upendo Kwao.
Umasikini Ni Mbaya, Ukiwa Masikini Hata Kama Una Upendo, Basi Upendo Wako Hautaonekana Kama Ukiwa Huna Kitu Cha Kutoa.
👍👍Urafiki mzuri, ujirani mwema, mahusiano yenye afya ni zao la malezi bora lakini malezi bora hutoka kwa baba na mama ambao wanapendana
👍👍👍Urafiki mzuri, ujirani mwema, mahusiano yenye afya ni zao la malezi bora lakini malezi bora hutoka kwa baba na mama ambao wanapendana
Usiamini yale wanayoyasema watu mdomoni, maana sio uhalisia wa mioyo yao
Kila mtu anaweza akawa mwema mbele ya uso wako, lakini itahitaji urafiki wa kweli na uaminifu wa kutosha kwa mtu huyo kuwa mwema nyuma ya mgongo wako
Urafiki ni kitu cha thamani kubwa sana. Ukiwa na marafiki wa kweli unakuwa na manufaa mengi ikiwemo ushauri wa kimaendeleo ili kuendana nao. Unapokuwa na shida au raha marafiki ni watu wa kwanza kuwa na wewe. Hata hivyo ili kudumisha urafiki kunahitaji uvumilivu na gharama pia.
📌📌📌Urafiki wa kweli haupimwi kwa furaha pekee, bali kwa uwezo wa kuhisi maumivu ya mwenzako na kusimama nae wakati wa changamoto. Huo ndio urafiki unaogusa moyo na kuacha alama ya kudumu maishani