UKIKUTANA NAYE UFANYE
Kwanza kaa ukijua fisi sio mnyama wa
kumchezea, naye ana uwezo wa kukurarua vile
vile, usijeanza fikiria zile hadithi za shule ya
msingi ukamchukulia pia, sungura mwenyewe
akimuona anafungua njia vibaya sana,
japokuwa si kiumbe anayevamia moja kwa
moja, huuma kwa kuvizia, jihami vya kutosha
na uwe na silaha nzuri kama fimbo nzito, mawe
yenye ujazo mzito, na usimpe nafasi ya
kumuonesha unamuogopa japokuwa kicheko
chake chaweza kukutia hofu Mara dufu.