Uzi maalum wa kutafuta mchumba. Weka Wasifu wako hapa upate wa kuanza naye maisha (njoo tuishi/tuyajenge)

Uzi maalum wa kutafuta mchumba. Weka Wasifu wako hapa upate wa kuanza naye maisha (njoo tuishi/tuyajenge)

NOT A JOKE! VERY SERIOUS.

Umri : 32
Elimu 😀igrii
KAZI:Nimejiajiri
Dini : Mkristo
Rangi: Mweusi
Urefu : wastani
Eneo : Kanda ya ziwa.
Sijawahi kuoa na sina mtoto.


NINAE MTAKA.

★Umri :18-26
★Dini :Mkristo
★Rangi : maji ya kunde/weupe wa kawaida
★Asiwe na mtoto (awe binti)
★Asiwe anajichubua.
★Elimu :kidato cha 4-digrii.
★Awe mnyenyekevu, mtiifu na mwelewa .
★Umbo sio kigezo sana japo asiwe na matiti makubwa na tumbo kubwaaaa.
★Urefu : We mrefu kiasi, asiwe mrefuu sanaa na asiwe mfupi.
★Akiwa muha itaongeza credit japo sio lazima awe Muha.

KIKUBWA AWE MWELEWA, BINTI AMBAE NAWEZA KUKAA NAE CHINI NIKAMWAMBIA HILI SIPENDI NA AKANIELEWA.


Alieko serious (usije kujaribu) aje pm. NIKIKUELEWA NAOA
 
Khaa, hii CV editing ni hatari, utafanya wachumba wote waje kwako jamani, sisi wengine tutaponea wapi sasa[emoji12],miaka 18 una degree 2, ulianza kusoma ukiwa tumboni wewe.[emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
2683228_JamiiForums1842265118.jpg

Kitu hicho
 
Habari wanajamvi hususani wanawake mlio singo na mnahitaji mwenza/mme wa maisha. Nami nimehamasika kuja uwanja huu kwani nimepata shuhuda kadhaa za waliofanikiwa kupata wenza humu jamvini.

Kiufupi nina kiu kubwa sana ya kupata mke kwa ajili ya kuanzisha na kuendeleza familia. Nishajipanga kimaisha na kisaikolojia.

Nina akili timamu na ninafahamu kuwa mwenza wa maisha anapatikana popote pale, tena nawashukuru waliotuletea platfom hii kutusaidia sisi ambao hatupati fursa hizi sehemu nyingine kwa sababu mbalimbali.

WASIFU WANGU
Jinsia; Me
Umri; Miaka 34
Kazi; Nimejiajiri pia nimeajiriwa
Elimu; Masters in Finance and Investment
Dini; Mkristo LC
Makazi; Dar Es Salaam

Mengineyo
Nina mwili wa wastani mrefu kiasi kimo futi 5 inchi 10, uzito kg 72. Sura ya kawaida na nina bald head( uwalaza)

Ni husband material kwa kwel, napenda sana familia, kujituma na kuwekeza ili kujiletea maendeleo


WASIFU WA NINAEMHITAJI

1. Umri awe miaka 25-30
2. Elimu angalau diploma
3. Kazi; Awe ameajiriwa/Kujiajiri. Ila hata kama hana kazi kwa sasa, nitamtafutia shughuli ya kufanya maana naamini katika kazi.
4. Dini; Napenda awe mkristo hususani dhehebu la LC, RC, au pentecoste
5.Makazi; Dsm, au awe tayari kuja kuishi Dsm
6.kabila; napendelea zaidi wa nyanda za juu kusini maana mmi ndio napotokea.
7. Awe na umbo la wastani, kama ni mnene asiwe mnene kupita kiasi

Mengineyo
Napenda mwanamke anaejitambua na anaejua wajibu wake kama mama wa familia

Napenda mwenye kiu ya maendeleo, asiwe mtu wa tamaa.

Napenda pia awe mshauri na mwenye kuona mbali kupitia ya leo(mwenye maono)


Nawakaribisha wenye nia. Karibuni


MAWASILIANO; PM YANGU IPO WAZI HADI NITAKAPOFANIKIWA

Sent using Jamii Forums mobile app
dini imeninyima mumeeeeeeeeee
 
Vigezo navyozingatia kwa atakae kuolewa
Mwanamke Muslim
Familia yake iwe ya kisalafi naye awe ktk manhaj hiyo awe amesoma dini na pia amesoma school education
Awe na check number (asiwe askari)
Miaka 21-30
Asiwe bonge
Urefu wa wastani
Maji ya kunde
Mzigua au
Msambaa au
Mbondei au
Myao
Ufafanuzi zaidi PM
 
Baada ya kuleta Uzi Huku WA kuvutana ndani, napendwa kutoa mrejesho kuwa nimepata nilichokuwa nahitaji na zaidi ya matarajio, nimepata mwanamke mzuri Kwa urembo na kichwani, anajua kujali, kupenda na kuheshimu...Kwa hakika jamii forum imejua kukifurahisha......Kwa wengine ambao MNA mrejesho mnaweza kuutoa pia, Kwa hakika jamii ni kiwanda cha kila kitu. Muwe na jumapili njema.
Ndoa lini mkuu?
 
Back
Top Bottom