Uzi maalumu kwaajili ya maombi ya Alfajiri

Nitafanyia kazi mkuu
 
Siku ya leo ikawe baraka kwako na kwa familia yako.

Haijalishi unapitia nini au upo hatua gani ya maisha Ila endelea kumshukuru MUNGU kwa kuamini kuwa mafanikio yako bado yanaishi.

Na ikiwa bwana atakupa kuendana basi akakupe kuendana kiroho na sio katika mwili utamanishao.

Barikiwa na hili ni ombi langu kwako

#NIFUNDISHE.




 
Tumaini letu ni kwamba, tusimame imara kwa bwana, na kumwamini kwa roho na kweli hatuta anguka,walio wake atawalinda, majaribuni atawaondoa, tumwamini na kutenda mema
 
Baba tunakushukuru kwa siku ya Leo

Tupo eneo hili kuiomba nguvu yako ikatawale katika maisha yetu

Nguvu yako ikawainue vitandani wagonjwa waliolazwa majumbani na hosptalini.

Nguvu yako ikawape tumaini jipya wafungwa waliopo vizuini na magerezani.

Nguvu yako ikawafanye viongozi wa nchi wakatuongoze kwa HEKIMA.

Na mwisho nguvu yako ikapate kuzibariki Kazi zetu za mikono .


Namshukuru alieanzisha Uzi huu kwani umefanyika Sana baraka na Mungu akakuinue tena na tena.🙏🏽
 
Nashukuru Mungu kumekucha tena ni siku nyingine mpya, ikawe siku ya baraka kwa kila mmoja wetu, milango ya mafanikio ifunguke tupate riziki kulingana na juhudi kwenye kazi zetu.

Kwa uwezo wa Mungu atuepushe na mikosi, balaa, laana na kila aina ya uovu uliopangwa juu yetu.

Utujalie afya njema, amani, furaha na moyo wa upendo kwa wengine, kwa namna ya pekee tuguswe kuyagusa maisha ya wengine hasa kujitoa sadaka kwa wahitaji. 🙏

Kila anaeamini na aseme AMEN, na ikawe siku njema.
 
Amen
 
Amina
 
Mpendwa hii picha nitaitumia katika maombi ya kesho
 
Amen
 

Amkeni katika maombi. Leo; maombi yenye majibu ya uhakika!. 1 Yohana 5:14-15; "Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa tukiomba kitu sawa sawa na mapenzi yake, atusikia. Tuombacho chote twajua kwamba tunazo zile haja tulizo muomba."
Mtumishi wa Bwana wasilisha maombi Kwa Bwana Kwa utulivu asubuhi ya Leo na uwe na uhakika ya kwamba umejibiwa, Tuendelee na maombi.
 
Asante MUNGU kwa siku nyingine tena,tunaomba ulinzi wako na nguvu zako zikatufunike siku hii ya leo ,ukatufanyie wepesi katika kazi zetu za mikono, na baraka zikawe mvua kwetu, tukiomba na kushukuru katika jina la YESU amina
 
Bwana, hatujui kilicho mbele yetu leo, lakini tunayakabidhi yote Kwako. Tafadhali tupe furaha na nguvu pia ujasiri wa kushinda kila lililo gumu mbele yetu, changamoto na matukio ya siku. Tunakushukuru kwa maisha yetu na vyote tulivyo navyo; Tunaikabidhi siku hii Kwako. Haijalishi nini kitatokea, tunajua Wewe ndie umetuweka katika kiganja cha mkono Wako kwa jila na utukufu wako wewe tunasema... Asante
 
Zaburi 90:14
Utushibishe asubuhi kwa fadhili zako. Nasi tutashangilia na kufurahi siku zetu zote.

Psalm 90:14
Oh, satisfy us early (in the morning) with Your mercy (steadfast love), That we may rejoice and be glad all our days!
 

Amkeni katika maombi. Mstari wa kusimamia. Philipi 4:6 "Msijisumbue Kwa neno lolote Bali katika Kila neno Kwa kusali na kuomba pamoja na kushukuru. Haja zenu na zijulikane Kwa Mungu."
Ubarikiwe mtumishi tuendelee na maombi pamoja na kushukuru karibu katika maombi ya Asubuhi.
Your browser is not able to play this audio.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…