Uzi maalumu kwaajili ya maombi ya Alfajiri

Zaburi 119:62
Katikati ya usiku nitaamka nikushukuru,
Kwa sababu ya hukumu zako za haki.
At midnight I will rise to give thanks unto thee because of thy righteous judgments.

Matendo ya Mitume 16:25-26
[25]Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza.
And at midnight Paul and Silas prayed, and sang praises unto God: and the prisoners heard them.

[26]Ghafula pakawa tetemeko kuu la nchi, hata misingi ya gereza ikatikisika, na mara hiyo milango ikafunguka, vifungo vya wote vikalegezwa.
And suddenly there was a great earthquake, so that the foundations of the prison were shaken: and immediately all the doors were opened, and every one's bands were loosed.
 
 
Asante Mungu kwa kutupa nafasi ambayo wengi wameikosa, tunashukuru kwa kuwa wazima tena tunaomba, ulinzi wako ukawe nasi tuweze kuimaliza siku hii salama, ukatushindie vita vya kiroho na kimwili dhidi ya maadui zetu, maana kwa nguvu zetu dhaifu hatuwezi chochote, tunaomba uwepo wako katika kila hatua zetu za kila siku, tukiomba hayo machache kupitia jina la mwanao Yesu kristo AMINA
 
Tunakushukuru kwa siku hii, kwa urafiki tunaoshiriki na wema mwingi wa mkate tunaomega pamoja. Mungu wa wema wote, tunaomba kwa shukrani kwa uwepo wako kati yetu tunapokusanyika pamoja, na ahadi yako ya kuwa nasi sasa na daima. AMINA
Zaburi 69 :30
italisifu jina la Mungu kwa wimbo,
Nami nitamtukuza kwa shukrani.
 
Ubarikiwe kuanzisha uzi mzuri sana...
 
Kesho tutakuwa na maombi ya kupata hakikisho la ulinzi wa Mungu

Kuna jambo nataka niseme na nyie wapendwa unapokuwa wewe mwenyewe faragha katika maombi ya usiku kama una jambo kwa muda mrefu halipati majibu anza sasa Leo kuomba kwa msisitizo neno moja ombea hata kwa mara kumi utaanza kuona matokeo Kuna ufahamu Mungu atauachilia kwako utapata urahisi wakutatua changamoto yoyote

Kwa wewe ambaye ukilala unatoa ndoto mbaya za shetani zile ndoto za kuota upo shuleni,unakula,unakimbizwa, unaingiliwa kimwili nk
anza kuomba hivi kwa msisitizo
"Kazi zote za shetani maishani mwangu nazikanyaga kwa damu ya Yesu"
"Mipango yote ya shetani naikataa kwa damu ya Yesu "

Omba hivi rudia ata mara 10 ukiwa katika Roho na kweli utaanza kuona matokeo

Tumepewa amri yakuharibu kazi za shetani
Luka 10:19
Zaburi 44:5
Zaburi 91:13

Kama umeota ndoto usiku ukawa haujaielewa ukiamka katika maombi muulize Roho Mtakatifu ndoto hiyo inamana gani Mungu atakupa majibu

Ndoto ni lango na ndio mana imeandikwa hivi

Waefeso 6:12
Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

Bwana Yesu awabariki sana
 
Kaka ubarikiwe
 

Ndugu hata huu Uzi tuufute tuu kwakuwa unakinzana na imani yako?

Just ignore him please. Atachoka na kwenda zake...maana mtakuja kuharibu huu uzi mzuri...na watu wa hivi huwa hawakosekani. Don't be so easily distracted. Please focus on the grace of God 🙏🏿
 
Amina tuendelee kujoin kwenye group la watsup ... Naogopa kuweka link humu nakumbuka ni unlawful
 
Amkeni katika maombi.
1 Wathethalonike 5 : 16 na 17. "Furahini siku zote" "ombeni bila kukoma"
Wapendwa Alfajiri ya Leo tunazidi kukumbushwa kuomba pasipo kukoma hivyo tuamke na tunyenyekee mbele zake kwaajili ya maombi, Amkeni tuendelee na maombi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…