Uzi maalumu kwaajili ya maombi ya Alfajiri

Uzi maalumu kwaajili ya maombi ya Alfajiri

Shalom shalom wapendwa
Bwana Yesu asifiwe

Ni siku nyingine tena namshukuru Mungu amenipa afya njema na kibali Nimeamka saa kumi na nusu kwa ajili kumtafuta BWANA nimefanya maombi ya kuombea watu wote,amani ya taifa letu,mamlaka zote, na pia nimefanya maombi kwa ajili ya mahitaji yangu nimebarikiwa sana

Kwa wale watu ambao wakilala usiku wanaota ndoto hizi risasi,mabomu au kula chakula hii ni ishara ya kuwa kuna adui ameona baraka zako zinakaribia hivyo anakuwa anajaribu kukuzuia kwa kutaka kukupa magonjwa au angamizo lolote ili mtu asifikie baraka isaya 29:8 isaya 54:17

Kuondokana na ndoto hizi ukimaliza kufanya maombi fungua biblia soma neno kutoka kitabu cha zaburi 91:1-6 soma neno lote ulishike lisitoke kinywani mwako ukifanya maombi ukatembea na neno ndivyo Mungu atakavyokupa majibu kwa haraka

Zaburi 91:1-6

Aketiye mahali pa siri pake Aliye juu Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.
2 Nitasema, Bwana ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu nitakayemtumaini.
3 Maana Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji, Na katika tauni iharibuyo.
4 Kwa manyoya yake atakufunika, Chini ya mbawa zake utapata kimbilio; Uaminifu wake ni ngao na kigao.
5 Hutaogopa hofu ya usiku, Wala mshale urukao mchana,
6 Wala tauni ipitayo gizani, Wala uele uharibuo adhuhuri,
 
Ndugu ubarikiwe sana sana
Shalom shalom wapendwa
Bwana Yesu asifiwe

Ni siku nyingine tena namshukuru Mungu amenipa afya njema na kibali Nimeamka saa kumi na nusu kwa ajili kumtafuta BWANA nimefanya maombi ya kuombea watu wote,amani ya taifa letu,mamlaka zote, na pia nimefanya maombi kwa ajili ya mahitaji yangu

Kwa wale watu ambao wakilala usiku wanaota ndoto hizi risasi,mabomu au kula chakula hii ni ishara ya kuwa kuna adui ameona baraka zako zinakaribia hivyo anakuwa anajaribu kukuzuia kwa kutaka kukupa magonjwa au angamizo lolote ili mtu asifikie baraka isaya 29:8 isaya 54:17

Kuondokana na ndoto hizi ukimaliza kufanya maombi fungua biblia soma neno kutoka kitabu cha zaburi 91:1-6 soma neno lote ulishike lisitoke kinywani mwako

Zaburi 91:1-6

Aketiye mahali pa siri pake Aliye juu Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.
2 Nitasema, Bwana ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu nitakayemtumaini.
3 Maana Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji, Na katika tauni iharibuyo.
4 Kwa manyoya yake atakufunika, Chini ya mbawa zake utapata kimbilio; Uaminifu wake ni ngao na kigao.
5 Hutaogopa hofu ya usiku, Wala mshale urukao mchana,
6 Wala tauni ipitayo gizani, Wala uele uharibuo adhuhuri,
 
Baba, asante tena kwa siku ya leo, sina namna nyingine ya kuja kwako ila kwa shukrani...
Asubuhi ya leo ni njema, na siku ya leo ni njema sana kwakua mapenzi yako na mipango yako mema ndio yatakayo timia siku ya leo.
Amen .
 
Ee Bwana, Baba yetu wa mbinguni, Mungu mwenyezi na wa milele, umetuleta salama hata mwanzo wa siku hii..... Ututetee kwa uweza wako mkuu, tusianguke katika dhambi wala tusiingie katika hatari yo yote. Na ili, tukiongozwa na Roho wako, tufanye yaliyo haki machoni pako Mungu uliye hai..... Amen
 
Wapendwa Kuna kitu nimekishangaa sana juu ya maombi. Mungu akiamua kukupambania kwenye jambo mapambano yake huwa ni "active" anapambana kweli kweli! Tusiache kudumu katika maombi ndugu zangu
Ipo nguvu kubwa katika maombi ya pamoja, na kupitia maombi ya pamoja mtu aliyekata tamaa hutiwa nguvu ya kuendelea kufanya maombi.
Maombi ya pamoja hufunika udhaifu wa mtu na kumtia nguvu.
Palipo na maombi ya pamoja upako au moto wa Roho Mtakatifu hushuka.
 
Habari za kwenu
Tunavyoingia kwenye maombi ya usiku na asubuhi wapendwa msisahau kufanya maombi kujipatanisha na Bwana Yesu kuombea watu wote wenye mamlaka hapa nchini mana shetani anavyotaka kumshusha mtu huwa anawatumia watu hawa wenye mamlaka kukuharibia
Tuombee viongozi Mungu awape hekima
Watu wote wenye mamlaka wafanye kazi kwa kutoa haki ikiwa ni mapolisi,majaji mahakamani, wakufanyaji wa Kodi nk

1 Timotheo 2:1-2
Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote;

[2]kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu.
.
 
Back
Top Bottom