Uzi maalumu kwaajili ya maombi ya Alfajiri

Bwana Yesu wapendwa
Msiwe mnapita kimya kwenye Uzi huu Mungu anasikia maombi yenu anajua mnahitaji nini na anatenda
Anawasikiza Ninyi tu mnaomba Nini
Mathayo 7:7
Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;
 
Naomba pia katika maombi yanayoendelea tuwakumbuke wagonjwa wote.
Tunakutana hapa kesho alfajiri
kwa maombi ya shukrani na kuombea watu wote wenye changamoto za kiafya wapo ambao pia wanauguza tutaendelea kuwaombea Mungu awape wepesi

Member wa uzi huu msilale sana hiyo mida unavyolala ndio muda unaompa shetani point 3 kuwahi kuamka na maombi ndio mwanzo wa kuiona nuru
 
Mungu wa Mbinguni,Muweza wa yote...usiyefananishwa na chochote wala Yeyote...Ninakushukuru kwa kutuamsha salama asubuhi ya leo tukiwa na UZIMA NA AFYA

Ahsante kwa Upendo wako

Ninakuomba uendelee kutulinda na kututunza, Pia ninakuomba uifanye siku ya leo iwe siku nzuri sana kwetu. AMEN.
 
Zab 138​

1 Nitakushukuru kwa moyo wangu wote,
Mbele ya miungu nitakuimbia zaburi.
2 Nitasujudu nikilikabili hekalu lako takatifu,
Nitalishukuru jina lako,
Kwa ajili ya fadhili zako na uaminifu wako,
Kwa maana umeikuza ahadi yako,
Kuliko jina lako lote.
3 Siku ile niliyokuita uliniitikia,
Ukanifariji nafsi kwa kunitia nguvu
 
Kesho tutafanya maombi maalumu ya kumuombea ndugu yetu @Uishmen Ambaye Kwa sasa anaumwa baada ya kupata ajali .

Maombi yatafanyika Ahsubui Jumamosi
 
Jambo jema kabisa imeandikwa muombeane Ninyi kwa Ninyi mana sala ya mtu mwenye haki yafaa sana akiomba kwa haki
Mungu anasema kuombea watu wengine jambo hili ni zuri lakubalika mbele zake Mungu mwokozi
Ambaye hutaka watu wote waokolewe
 
Tutakutana hapa kesho alfajiri kwa ajili ya kuomba rehema na toba pia tutamuombea na huyo mwenzetu aliyepata ajali
 
OK tuombe kheri Mungu akituamsha salama tukapte kumuombea kheri ndugu yetu.
Tutamaliza wiki hili kwa maombi ya shukrani na kumuombea member mwenzetu wa muda mrefu humu JF aliyepata ajari
Tutaongozwa na Neno kutoka kitabu cha wagalatia

Wagalatia 5:14
Maana torati yote imetimilika katika neno moja, nalo ni hili, Umpende jirani yako kama nafsi yako.
 
Nasubiri
 
"Zaburi 118: 17 sitakufa nami nitaishi na kuyasimulia matendo ya bwana "

Maombi haya ni maalumu kwa ndugu yetu Ushimen

Baba yetu tunakushukuru Kwa siku ya leo , tupo hapa katika kusanyiko hili kuomba neema yako ikawe juu yetu na nguvu yako ikayatawale maisha yetu.

Baba tunakuomba kampatie mtumishi wako Afya ya mwili damu na mifupa .

Sehemu yenye hapana ikawe ndio hakika ikiwa mtumishi wako ulimlimda dhidi ya umauti basi kamlinde dhidi ya maradhi yanayomsumbua .

Tunakuomba ukafinyike Nuru katika mtumishi wako yeye pamoja na familia yake.

"Mtumishi Ushimen amefanyika baraka Sana kwa watu wengi hivyo tusiache kumkubuka katika sala zetu pamoja na dua "

Mungu ni mwaminifu Sana atatenda na ametenda.
 
Gulio Tanzania
cacutee
Mshana Jr
 
Amen Baba wa Mbinguni uyapokee maombi yetu
 
Back
Top Bottom