Uzi maalumu wa kujua gharama za ujenzi wa majengo mbalimbali

Namba ya vyumba haiwez saidia sana kujua makadirio bila raman..mimi naweza jenga nyumba yenye ukubwa wa 14 Γ— 16 na ikawa na vyumba vitatu tuu na mwingine akajenga nyumba ya 13 x 14 na ikawa vyumba vinne, hivyo yenye vyumba vitatu ikawa nyumba kubwa na gharama zaid kuliko ile ya vyumba vinne..ukisema tuu vyumba vitatu bila kujua ukubwa wa vyumba, ukubwa wa sebure, ukubwa wa Jiko itakuwa uongo
 
NYumba zatofautiana ubora. Ya kwake 122 nyumba moja..wewe unatoa mbili, mwingine anatoa hata 5 kwa bei hiyo hiyo
 
Hapo kama umeshaweka plan za spanish, german hiyo sio nyumba simpo tena ni bajeti kwelikweli uandae..otherwise ukutane na matapeli wakupe mchina wakikudanganya ni mjerumani
 
Mimi nilijenga nyumba ya 4 bedrooms na kwa specifications karibu sawa na ulizotoa hapo juu mwaka 2019 hapa Iringa. Gharama zote na kuingia ndani kuishi ikiwa complete kwa matofali ya block ya cement nilitumia 122,000,000/-

Uzembe wako usikatishe tamaa wengine!,inaonekana pesa unapata za kupiga kiraihisi rahisi ndio maana unaweza kupigwa kiasi hicho lkn sio gharama halisi
 
Kama utamkwepa mchina hakuna namna hautofika 100m au kuikaribia na pengine huenda ukazidi hiyo by far. No way
 
Msaada ppt
 
NYumba zatofautiana ubora. Ya kwake 122 nyumba moja..wewe unatoa mbili, mwingine anatoa hata 5 kwa bei hiyo hiyo
Kabisa kwa watu wasiowai kujenga hawawezi kuelewa.

Nyumba zinatofautiana ubora kabisa.

-Kuna mwingine atatumia tofali zenye mawe nchi 6 ,mwingine atatumia tofali ubuyu za nchi 5
-Mwingine atatumia nondo za 12mm kupiga mkanda ,mwingine 16mm ,mwingine hafungi mkanda kabisa au mwingine anapiga jamvi.
-Mwingine Mkanda anaweka 6" ,mwingine mkanda 8"
-Mwingine atatumia kokoto za msolwa ,mwingine atatumia ubuyu wa kunduchi mtongani.
-Mwingine atatumia tywod tiles ,mwingine atatumia spanish
-Mwingine attumia mbao treated ,mwingine atatumia mbao zilipigwa rangi ya ukili.
-Mwingine atatumia Gypsum za Thailand ,mwingine atatumia BBG.
-Mwingine atatumia rangi ya Billion au Matemba ,Mwingine atatumia Goldstar.
-Mwingine atatumia SSP ,mwingine atatumia Andika Powder.
-Mwingine atatumia Milango ya mninga ,mwingine atatumia milango "seplasi" iliyopigwa rangi ya mchongo.
-Mwingine atatumia kitasa cha orando ,mwingine Obama.
-Mwingien atatumia drewa ,mwingine weather guard
-Mwingine madirisha atapiga flat bar ,mwingine atapiga nondo.
-Mwingine atatumia alaf ,mwingine bati bomba

Kwahiyo umeeleza ukweli yeye ametumia 122m kujenga hiyo nyumba ,kuna wengine kina Jimmy Mafufu alitumia zaidi ya 200m na nyumba bado haijaisha na pia akienda kule charambe kwenye jenga uza hiyo 122m anaweza kujenga hata 7.
 
Hongera mkuu. Mimi huwa napenda sana watu wanaofanya vitu vya maendeleo.
 
Hili desa limejaa madini kibao. Umedadavua kinagaubaga. Umegusa kotekote low vs full budget
 
Mimi nilijenga nyumba ya 4 bedrooms na kwa specifications karibu sawa na ulizotoa hapo juu mwaka 2019 hapa Iringa. Gharama zote na kuingia ndani kuishi ikiwa complete kwa matofali ya block ya cement nilitumia 122,000,000/-
Mi nakuelewa nimejenga nyumba vyumba vinne mwaka huu ndio namalizia gharama zimepanda sana imefika zaidi ya milioni 150. Watu watabisha ila huo ndio ukweli.

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…