Uzi maridadi kabisa nimeupenda, napenda kuishi maisha flani yasiyopoteza ladha ya kiafrika km kula vyakula asili, kutumia dawa asili nk
Nafahamu baadhi ya dawa ila nyingine sijui majina kwa kiswahili labda kwa kilugha cha kwetu,
Dawa ya kinyama cha jicho, sijui ndo wanaita kansa ya macho,, ni mti flani unauzwa sana na taasisi za kidini niliwahi kusikia wanasema eti ni moja mti ulikuwepo ktk bustani ya Eden,, akipatikana anaeujua huu mti atume picha yake, kwa jina la kilugha unaitwa, 'OMUHUHE'
Matumizi ni kama ifuatavyo; unachuma majani yake yaliyo machanga,, unayaosha na kuosha utakapopondea,, hakikisha yanalainika kabisa, then unayafunga vizuri kwenye jani la mgomba,, kama wauza karanga au unga wanavyofungasha unga mchele kwenye gazeti, kisha unabinya dawa uliyoponda ili kutoa maji ya dawa husika, hakikisha maji yanadondokea sehemu safi yaweza kuwa kisosi au kibakuli kidogo tu, baada ya hapo unatafuta mirija ya kienyeji, yapo majani huwa yanakuwa na uwazi katikati,(wazee zamani walitumia kunywea pombe), unavuta hiyo dawa kwenye mrija huo ukihisi imepanda unazuia kwa kidole ili isimwagike,, halafu unamdondoshea mgonjwa kwenye macho,,, fanya hivi kwa kurudia katika miezi 3-6 kutegemea na ukubwa wa kinyama,, kitaisha
Hii dawa niliwahi kutibia mtu aliyekuwa na kinyama kilikuwa kinaonekana kabisa, hakikuwa kinamuuma, siku moja akaamua kwenda hospital wakamwambia ni kinyama na alitakiwa kufanyiwa upasuaji haraka maana alikuwa anaelekea kuwa kipofu, ndipo tukaambiwa hiyo dawa na alipona hadi leo hakijarudi
Tangu hapa niliheshimu mitishamba na nilianza kuitilia maanani