Uzi maalumu wa Mimea Tiba inayotuzunguka majumbani

Uzi maalumu wa Mimea Tiba inayotuzunguka majumbani

Wakuu naomba kufahamu dawa za mimea yetu ya asili zinayotibu MIGUU NA MIKONO KUWAKA MOTO na MIGUU NA MIKONO KUFA GANZI(PERIPHERAL NEUROPATHY na LEG NUMBNESS)
Natanguliza shukran
 
Majani ya matunda na maganda ya matunda tuyatumiayo mara nyingi nayo huwa na viini dawa muhimu kwa miili yetu:-
Hutumika kama chai bila kuwekwa sukari,
°MAJANI YA MWEMBE:-
Chai yake hausaidia sana katika kurekebisha mfumo wa fahamu.
°MAJANI YA MPERA:-
Husaidia kupambana na kansa, kisukari, cholesral, inaondoa chunks na kutengeneza ngozi.
°MAJANI YA PARACHICHI:-
Husaidia uti wa mgongo kurekebisha utendaji kazi
°MAJANI YA MORINGA:-
Haya hutibu zaidi ya magonjwa 300 ya mwili wa binadamu.
°MAJANI YA MNANASI:-
Yanasaidia kutibu vidonda vya tumbo, kuondoa sumu mwilini, na maumivu ya mwili.
 
Weka kipande cha amdalasini mfukoni katika waleti yake, kila asubuhi utamkage "YA HAKUL" MARA MIA MOJA, nenda kwenye mishe zako, Nimekupa huduma ya kwanza ndg.baada ya siku 40 utafurahi sana.
Asante sana mkuu. Nina nahitaji ufafanuzi katika vipengele hivi Ili nielewe vizuri

i)Je, ni kipande kimoja (gome) au Hata hii ya unga unga inatosha?


ii) Je, nitamke kwa sauti au Hata kimya kimya inafaa?

iii) Je, hicho kipande cha mdalasini nitemebee nacho?
 
Asante sana mkuu. Nina nahitaji ufafanuzi katika vipengele hivi Ili nielewe vizuri

i)Je, ni kipande kimoja (gome) au Hata hii ya unga unga inatosha?


ii) Je, nitamke kwa sauti au Hata kimya kimya inafaa?

iii) Je, hicho kipande cha mdalasini nitemebee nacho?
Tumia vipande viwili vya mdlasini weka kwenye wallet vikae humo, asubuhi tamka hayo maneno kimya kimya ukiweza na jioni kwa ufanisi zaidi.
*ngazi ya kwanza hii.
 
Tumia vipande viwili vya mdlasini weka kwenye wallet vikae humo, asubuhi tamka hayo maneno kimya kimya ukiweza na jioni kwa ufanisi zaidi.
Nashukuru sana mkuu.
Hata nisipotembea nayo wallet yenyewe ikawa ya ndani tu ni Sawa?? Au yatakiwa niwe natembea nayo? Maana mimi na wallet ni kama serikali ya Tz na bhange
 
Uzi maridadi kabisa nimeupenda, napenda kuishi maisha flani yasiyopoteza ladha ya kiafrika km kula vyakula asili, kutumia dawa asili nk

Nafahamu baadhi ya dawa ila nyingine sijui majina kwa kiswahili labda kwa kilugha cha kwetu,
Dawa ya kinyama cha jicho, sijui ndo wanaita kansa ya macho,, ni mti flani unauzwa sana na taasisi za kidini niliwahi kusikia wanasema eti ni moja mti ulikuwepo ktk bustani ya Eden,, akipatikana anaeujua huu mti atume picha yake, kwa jina la kilugha unaitwa, 'OMUHUHE'

Matumizi ni kama ifuatavyo; unachuma majani yake yaliyo machanga,, unayaosha na kuosha utakapopondea,, hakikisha yanalainika kabisa, then unayafunga vizuri kwenye jani la mgomba,, kama wauza karanga au unga wanavyofungasha unga mchele kwenye gazeti, kisha unabinya dawa uliyoponda ili kutoa maji ya dawa husika, hakikisha maji yanadondokea sehemu safi yaweza kuwa kisosi au kibakuli kidogo tu, baada ya hapo unatafuta mirija ya kienyeji, yapo majani huwa yanakuwa na uwazi katikati,(wazee zamani walitumia kunywea pombe), unavuta hiyo dawa kwenye mrija huo ukihisi imepanda unazuia kwa kidole ili isimwagike,, halafu unamdondoshea mgonjwa kwenye macho,,, fanya hivi kwa kurudia katika miezi 3-6 kutegemea na ukubwa wa kinyama,, kitaisha

Hii dawa niliwahi kutibia mtu aliyekuwa na kinyama kilikuwa kinaonekana kabisa, hakikuwa kinamuuma, siku moja akaamua kwenda hospital wakamwambia ni kinyama na alitakiwa kufanyiwa upasuaji haraka maana alikuwa anaelekea kuwa kipofu, ndipo tukaambiwa hiyo dawa na alipona hadi leo hakijarudi

Tangu hapa niliheshimu mitishamba na nilianza kuitilia maanani

Sorry, ni kabila gani tuweze kiufuatilia hukooo jikoni, kikubwa umetupatia jina.
 
Back
Top Bottom