UZI MAALUMU: Wanawake wote ambao wana msongo wa mawazo kwa sababu ya kutoolewa mkutane hapa

usiwaumize hao dada zetu, unawatonesha kidonda. kiukweli, hakuna mwanamke hata kama angekuwa amekuwa mtembezi kwa wanaume wengi, asiyependa kuolewa. wachache sana hawataki kuolewa na hao wana mapepo. wazazi pia tunapenda mabinti zetu waolewe, tunapenda dada zetu waolewe, ili wapate ndoa, ni heshima, kuchelewa kuolewa ni ajali tu kazini inayoweza kumpata mtu yeyote, ni kama ajali ya ugonjwa tu au ajali barabarani, hakuna anayependa ila inatokea inamkuta mtu, wanahitaji faraja, wanahitaji kutiwa moyo na kupewa matumaini, sio kuvunjwa moyo au kuwasema. kama una mabinti tema mate chini, waombee hao dada zetu kuliko kuwasimanga. tena most of them wamepoteza muda kwenye masomo wakitafuta pa kujishikiza.
 
Kasome vizuri uzi lengo la thread hakuna anayesimangwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…