Uzi wa sehemu za gharama nafuu kulala kwa wanaokwenda kwenye saili Dodoma

Uzi wa sehemu za gharama nafuu kulala kwa wanaokwenda kwenye saili Dodoma

Wakuu mambo vipi? Naona ma PDF yameanza kumwagika, changamoto ya malalamiko ya kwanini Utumishi wako kimya, inakwenda kuisha huku changamoto nyingine zinazotokana na kuitwa zinaanza kuibuka kwa kasi ya ajabu. Hii ni kwa wote, wanaokwenda kwenye Saili mbalimbali na hata wanaowategemea.

Tafadhali, naomba tutumie uzi huu kwa kutaja, nyumba za wageni ambazo ni rahisi mtu kukaa na kufika eneo la Usaili kwa gharama ndogo, maeneo zilipo, gharama na hata mawasiliano kama yapo. Hii itasaidia wengi hasa wanaokwenda kwenye Saili Dodoma kwa mara ya kwanza, au hata waliowahi kwenda na wakaishia kuteseka.

NB: Japo sio kwa umuhimu, inasemekana wengine hulala nje, baa na maeneo mengine kwa kutokuwa na pesa kabisa. Kama hayo maeneo yapo na ni salama naomba tusaidiane kuyataja ili watakaojikuta hali haziruhusu wakimbilie huko.

Asante.
Kwa pisi kali ambazo zinakuja kwa interview na hazina pa kufika, basi waseme hapa, nafasi ni chache.
 
kama huna pesa safiri jioni fika dodoma usiku, lala stendi kuu ya mabasi pale ni salama na jengo la kulala ni zuri mtakutana wengi tu. Alafu asubuhi anza kufanya safari yako kwenda mahali pa usaili ulipopangiwa. kwa usafiri wowote huwezi tumia dakika zaidi ya 30 kutoka stendi kwenda mahali ulipopangiwa usaili.
Lile baridi la Dodoma ni la kulala nje kweli?
 
Kwa pisi kali ambazo zinakuja kwa interview na hazina pa kufika, basi waseme hapa, nafasi ni chache.

Hahaha! Duh! Sawa Mkuu, nashauri uambatanishe na maelezo ya ziada, ikiwemo uko Dodoma sehemu gani, na watafikia kwako binafasi au unautaratibu wa kuwatafutia loji.

Kama itakufaa, naomba pia uweke wazi wewe watakuwa wanakulipa nini, na pisi kali kwako inatakiwa ziwe na sifa gani.
 
Hahahaa, mimi nina nalea huku home, nikirudi huduma kama hiyo naipata vizuri tu.

Huku nawaachieni wengine wenye bachelor mbili[emoji3]

Hahaha, sawa Mkuu. Japo ilikuwa ni nafasi mzuri ya kubadilisha mawazo na Mkuu moneytalk.
 
Back
Top Bottom