Ukiondoka hapo kwa shemeji utapata kazi,angalau ya kukuwezesha kula;kuendelea kubaki hapo inamaanisha kuna baadhi ya kazi unabagua
Amesema kwa shemeji ana amani na kila kitu anapata, ni ngumu sana kwa mtu wa hv kuwaza inje ya box maana hata kazi atakuwa anachagua na vibarua ataona sio hadhi yake. Lkn angekuwa anaishi kwa kudaiwa kodi, umeme, maji, na huku huna uhakika wa mkono kwenda kinywani, angepata shughuli ya kufanya.
Nilichojifunza katika maisha kwa miaka yangu yote 35 hapa duniani ni kwamba, anayekufanyia roho mbaya, anayekunyanyasa ndio anakufundisha maisha, ndie anakupa akili ya kutafuta any means uweze kusimama na ndie anayekupa ujasiri wa kupambana na lolote linalokuja mbele yako hata liwe gunu kiasi gani.
Hao wanaotulea na kutuonea huruma mara nyingi ndio wanatudumaza na kutufanya tushindwe kujitegemea.
Kama dada yako anauchungu na maisha yako anapenda ufanikiwe angekupa hata mtaji kidogo ukajishughulishe si wana uwezo? Lkn amekuacha mwaka wa tatu huu unamtegemea yeye na umri huo 28 kweli? Au ndio ukitaka kwenda kujitegemea anakwambia kwani hapa unakosa nini?
Maisha ni zaidi ya kula na kulala na usiogope kutoka eti utakwama, mikwamo ndio maisha yenyewe, unakwama ili akili ifanye kazi..