@Mshana Jr umenifanya nikumbuke mbali sana....
Ni kati ya mwaka 2006 na 2008 kipindi niko secondary huko Shinyanga. Shybush kwa utani.. kulitokea mwamba akasepa na kitita Changu ilikuwa ni laki 3 bwana nimempanga mzee na nimekuja nayo shule... sasa Ile peered pressure nikaamua niende maganzo kumtafuta witch doctor [emoji16] nikapewa maelekezo kuwa kuna kijiji kimoja kipo maeneo ya ibadakuli kuwa kuna Bibi kizee ni hatari kubwa... wakati huo hata siamini kama wanaweza kunisaidia...
[emoji851][emoji851]Duuh Yaani mzee kwa mara ya Kwanza naona television screen kwenye beseni Yaani mchezo wote utadhani Movie... [emoji15]duuh Yaani bedmate wangu ndo alinifanyia huo wizi....Halafu mzee akaniuliza unataka nimfanye nini?? Yaani moyo Ulikuwa unadunda vibaya sana. Nilimuomba tu aache kumdhuru na niliweka Buku 5 kwenye kijichungu fulani hivi...
Uchawi Upo wakuu [emoji3064][emoji3064][emoji3064]