Vazi la Makonda lazua mjadala hapa Moshi

Vazi la Makonda lazua mjadala hapa Moshi

Hivi Bashite alikuwa pale kama nani mpaka akapewa tena Nafasi ya kuongea? Watanzania huu uoga na unafiki utatupeleka kubaya.

Bashite alishapewa Nafasi ya kuongea Dar kama RC na akaongea alichokiongea. Kwa kweli hakustahiki second chance. Pamoja na kupewa bado hakuitumia vizuri..... Ni arrogance at its best.
 
Mh, nabaki najiuliza....
1. Ilikuwaje akachaguliwa kuwa kiongozi?
2. Na huyo aliyemchagua alitumia kigezo gani?
3. Je haya yote anayofanya huyu jamaa, Mkubwa hayaoni au?
4. Kuna uhusiano gani uliojificha kati ya huyu jamaa na mkubwa?
Inasemekana ndio mbeba vibuyu vya kinga za mkubwa hivyo ni ngumu kumtumbua.
 
Baba Askofu alimwita madhabahuni ili ampatanishe na Mboe,kibwana mdogo kikawa kinagoma kujongea mbele
Ingekua bora zaidi kutokwenda, aliharibu zaidi baada ya kwenda madhabahuni na kutaka kuanzisha majibishano kila mtu alimdharau, mbaya zaidi alipopewa nafasi ya kuongea katika kutoa salam watu wote walikaa kimya.... aibuuuuuuuuuuu kondaaaaa
 
Labda Hiyo Jinsi ilichanika kwa bahati mbaya akiwa safarini kuelekea msibani.
Siamini kama binafsi alidhamiria kuivaa.
Yaani avae jinsi iliyochanika kwa makusudi...!
Labda sio Makonda.
Au Picha ime editiwa...!
 
Hakuna mkuu wa wilaya/mkoa yeyote amngeweza kuvaa vile achilia mbali hata mwananchi wa kawaida lazima ujitafakari lakini yeye katinga hivyo hivyo! Duuuh kweli akili ni Mali
Hata disco huweza kwenda kwa staili ya vile. Inaonekana leo kaamka na mapepo
 
Kwahiyo wazungu ndo wa kuwekewa mfano??

Faken wallah
Wazungu ndio SI Unit ya ustaarabu au kama unabisha rudi kwenye tamaduni za kibantu. Hiyo simu choma moto, hizo nguo tupa zote , kavae magome ya miti.
 
Washamba wamepewa nchi. Jamaa ndio vitu kavijua sasa, full ulimbukeni.
 
Leo Mkuu wa Mkoa wa Dar ameingia ibadani katika kanisa kuu la KKKT hapa Moshi akiwa amevaa Suruali iliyozua minong'ono kuwa ya KIHUNI.

Baadhi ya Waumini waliopo hapa Ibadani wamesikika wakiuliza je angekufa babake angekwenda na vazi kama hilo?

Wengine walisikika wakisema vazi hilo hata katika mavazi yanayotakiwa kwenye Ofisi za Umma hayatakiwi iweje avae kanisani?

Waumini wengi wamesikika wakihoji kiwango cha nidhamu alichoonyesha Mkuu huyu kupitia vazi lake.View attachment 1092613
Wanaume wa Dar bana kwani akivaa hivyo kuna shida gani? Acha wazee waendelee kuwatambia mjini maana hamjiwezi.
 
Leo Mkuu wa Mkoa wa Dar ameingia ibadani katika kanisa kuu la KKKT hapa Moshi akiwa amevaa Suruali iliyozua minong'ono kuwa ya KIHUNI.

Baadhi ya Waumini waliopo hapa Ibadani wamesikika wakiuliza je angekufa babake angekwenda na vazi kama hilo?

Wengine walisikika wakisema vazi hilo hata katika mavazi yanayotakiwa kwenye Ofisi za Umma hayatakiwi iweje avae kanisani?

Waumini wengi wamesikika wakihoji kiwango cha nidhamu alichoonyesha Mkuu huyu kupitia vazi lake.View attachment 1092613
Vitu alivyopaswa kuvifanya wakati wa balehe ya kwanza yeye anavifanya ukubwani tena katika muktadja ambao hata chizi lazima awe na staha.tatizo madaraka siyo mtu mwenyewe
 
Mimi naona sijui utandawazi,zamani wakati tunafukia kwa kifusi cha udongo hizo nguo alizovaa ndiyo zinatakiwa.Kwa kuwa wanajamii hawampendi Mhe.ndiyo wanapanga alitakiwa avae vazi gani.Mimi pia huwa nashangaa watu wamevaa misuti na tai wamekaa kwenye viti.Halafu wale maskini wenzangu ndiyo wanasimamia/shiriki maziko mwanzo mwisho.
 
Back
Top Bottom