Wamachinga huwa wanapenda kukaa sehem zenye mkusanyiko wa watu wengi hasa wale ambao wapo katika movement kubwa ya kutoka sehem moja kwenda nyingine.
Kwa jiji la Dar es Salaam sasa hivi jinsi lilivyo inahitajika kubuni stendi kubwa nyingi sanaa na kuhakikisha daladala za kwenda sehem mbalimbali zinakutana katika hizo stendi.
Mfano stendi kama Kariakoo, Mnazi Mmoja, Posta(Bandarini na Stesheni), Makumbusho, Mwenge, Mbagala rangi 3, Ubungo, Tabata, Buguruni, Temeke, Tandika, Kigamboni, Gongo la mboto, Tegeta, Mbezi na maeneo mengi ambayo yanakuwa na movements ya watu wengi.
Stendi zijengwe kwa kuwezesha daladala ziwe zinalazimika kuwamwaga watu hapo na hapo wanatakiwa kuunganisha safari zao bila ya kutembea tena umbali mwingine kufuata daladala zingine.
Hii itasaidia sana kuwaondoa wale wamachinga wanao jipanga kando ya barabara kuvizia hizo movements za watu.
Kingine mfano wa stendi ya makumbusho pale hakuna wamachinga wengi wamejipanga kando kando ya barabara za kuingia kuelekea stendi sababu hawana huo ulazima. Wamachinga wengi wapo ndani mule stendi wamejibana.
Mtu hawezi kushuka ndani ya gari huku mwanzoni mwa zile barabara zinazotumiwa na daladala kuingia stendi ya makumbusho kisa tu anunue kitu ambacho akifika ndani mule stendi anaweza kukipata na akaunga Safari yake bila usumbufu.
Wamachinga wateja wao ni watu ambao wananunua vitu kwa kushtukiza yaani, ameona bidhaa rahisi kubebeka na akaona kule nyumbani sina hiko kitu basi ananunua na kuendelea na safari yake.
Tofuati na hayo ma Mall na Supermarket ambapo mteja huwa anajipanga kabisa kuwa naenda kufanya shopping sehemu fulani.
Kwahiyo kusema wamachinga wakusanyike sehemu sijui kama machinga Complex pale hakuna movement ya watu ya kueleweka ni kama kuwafanya wajiwekee kishopping Mall chao na kamwe hawawezi kupata wateja wao wa siku zote ambao ni watu wapita njia tu.