Vibanda vilivyowekwa kando ya barabara Jijini Dar es Salaam kuondolewa

Vibanda vilivyowekwa kando ya barabara Jijini Dar es Salaam kuondolewa

Wenye Mabanda yote kando ya barabara wametakiwa kuyabomoa kabla ya tarehe 18 mwezi huu ambapo ndio tarehe ya bomoabomoa. Mtakumbuka jinsi mabanda yayivyokua yameshamiri kila pande ya jiji na kuharibu kabisa muonekano wa mji kama miji minginge mikubwa ya majiran zetu hadi kufikia kuonekana jiji lote ni slum. Kuanzia maeneo ya fire,DIT hadi kisutu ilikua kituko hata kupishana watembea kwa miguu ni shida. Mlimani city ndio usiseme kabisa. Angalau jiji litaanza kuonekana sasa maana moshi wa mamantilie wanaopikia kuni pembeni ya barabara ndo ulikua unaonekana.Yaani hata Nairobi au Kigali tu walikua wanaonekana wametuacha mbali kisa haya mabanda maana kila mtu kajenga anavyojua na kuezeka anavyojua. Dar inarudi kuwa Dar
Hapa sijakuelewa mkuu.
Ni Dar mkoa ua Dar jiji? Ikiwa ni Dar mkoa sawa, lakini kama ni Dar Jiji sisi temeke, kinondoni na kigamboni hatumo kwenye operesheni hiyo na tena haituhusu
 
Aisee Arusha hali mbaya zaidi nadhani yule mshenzy mla nyama za watu alifanya makusudi akihofia uchaguzi wa 2020, jitu jinga sana lile ndo maana likafa!
Ni mjinga tu atakesimanga kifo chako!!
 
HIVI MSAJILI HAWAWEZI KU SCARIFY MAGOROFA MATATU TU KARIAKOO YALIYOFUATANA IKATENGENEZWA MALL KUBWA KWELI YA GHOROFA 10 IKAJENGWA KWA UFUNDI NA RAMANI YA AINA YAKE IKABEBA MACHINGA 10,000 WALIOPO KARIAKOO SEREKALI IKAWA INAPATA KODI YAKE KWA WEPESI?,MAANA MACHINGA WAMEIKOMALIA SANA KARIAKOO NA KUWAFUKUZA WAKATI MWINGINE SIO HAKI,PIA KUWAHAMISHA INAKUWA NGUMU,KARUME PABAKIE,ILALA,PABAKIE,MACHINGA COMPLEX ISANIFIWE IBADILISHWE ILI YAWE MAKAZI NA FIDIA KWA MAJENGO MATATU WATAKAYOWAPA JIJI KATIKA UJENZI WA MALL.
Hio hata mtu binafsi anaweza fanya hivo ila machinga ni kama mtoto mchafu raha yake uchafu.Kuzagaa ndo raha yao ili waonekane wako busy
 
Kwa hiyo ni Bora iwe rasimi sasa, embu umefikiri Kwamba, Ikiwa itakuwa hivyo, na Kwa sifa mbaya tuliyonayo Watanzania kuwa,Sisi ni wavivu, waizi maofisini ingawa sio wote, Je, ni Watanzania wangapi watapoteza ajira zao baada ya tangazo Hilo??
Kwanini upoteze ajira kwa kuzembea kazi wakati kuna watu wanataka kufanya kazi hiyo? kuwajibika katika shughuli yeyote ile ni lengo la kupata manufaa zaidi na kujiongezea tija na ari kwa jamii inayokuzunguka, Kwanini hujiulizi mbona wengine wanapanda cheo au kuongezewa mshahara na wengine hapana.
 
Mitaa ya miji yooote Tanzania imegeuzwa masoko yasiyo na mpangilio wa aina yoyote. Watu tunatafuta riziki, lakini siyo kila eneo la wazi au waenda miguu kugeuzwa masoko, majiko n.k. Tatizo la ajira lipatiwe ufumbuzi kwa kuvutia wawekezaji wa nje na ndani kuzalisha ajira rasmi na siyo njia ya mkato kugeuzwa mitaa yote mijini kuwa masoko.
 
HIVI MSAJILI HAWAWEZI KU SCARIFY MAGOROFA MATATU TU KARIAKOO YALIYOFUATANA IKATENGENEZWA MALL KUBWA KWELI YA GHOROFA 10 IKAJENGWA KWA UFUNDI NA RAMANI YA AINA YAKE IKABEBA MACHINGA 10,000 WALIOPO KARIAKOO SEREKALI IKAWA INAPATA KODI YAKE KWA WEPESI?,MAANA MACHINGA WAMEIKOMALIA SANA KARIAKOO NA KUWAFUKUZA WAKATI MWINGINE SIO HAKI,PIA KUWAHAMISHA INAKUWA NGUMU,KARUME PABAKIE,ILALA,PABAKIE,MACHINGA COMPLEX ISANIFIWE IBADILISHWE ILI YAWE MAKAZI NA FIDIA KWA MAJENGO MATATU WATAKAYOWAPA JIJI KATIKA UJENZI WA MALL.
Ile Machinga Complex imejaa mkuu? Wamachinga hawaitaji gorofa mkuu.
 
Mkuu mbona hii kama haipo specifically, ni barabara kuu za lami au mpk barabara za vumbi za ndani ndani zilizo chini ya tanrod?
 
Kwanini upoteze ajira kwa kuzembea kazi wakati kuna watu wanataka kufanya kazi hiyo? kuwajibika katika shughuli yeyote ile ni lengo la kupata manufaa zaidi na kujiongezea tija na ari kwa jamii inayokuzunguka, Kwanini hujiulizi mbona wengine wanapanda cheo au kuongezewa mshahara na wengine hapana.
Sina hakika kama ilikuwa ni tamaa yangu pekee nilipoamua kujitanua na kwenda kufungua kakampuni kangu nchi jirani, nikitamani nifanye na Watanzania tu, lkn Kwa mjibu wa sheria za nchi Hiyo, haikuwezekana, nikashindwa Fanya hivyo,

Sasa, jiulize, ni watu wangapi wenye mawazo kama yangu ambao watakuja hapa nchini, huoni Kwamba ajira zitapukutika mkuu
 
Back
Top Bottom