Vibanda vilivyowekwa kando ya barabara Jijini Dar es Salaam kuondolewa

Vibanda vilivyowekwa kando ya barabara Jijini Dar es Salaam kuondolewa

Gari la tangazo linapita kutangaza ya kuwa ifikapo tarehe 18 mwezi huu hakitakiwi kibanda chochote kuonekana kando kando ya barabara katika jiji la Dar es salaam.
UKIHAMA ULIPOPANGA KABLA YA KUJENGA NYUMBA YAKO USILALAMIKE
 
Wenye Mabanda yote kando ya barabara wametakiwa kuyabomoa kabla ya tarehe 18 mwezi huu ambapo ndio tarehe ya bomoabomoa. Mtakumbuka jinsi mabanda yayivyokua yameshamiri kila pande ya jiji na kuharibu kabisa muonekano wa mji kama miji minginge mikubwa ya majiran zetu hadi kufikia kuonekana jiji lote ni slum. Kuanzia maeneo ya fire,DIT hadi kisutu ilikua kituko hata kupishana watembea kwa miguu ni shida. Mlimani city ndio usiseme kabisa. Angalau jiji litaanza kuonekana sasa maana moshi wa mamantilie wanaopikia kuni pembeni ya barabara ndo ulikua unaonekana.Yaani hata Nairobi au Kigali tu walikua wanaonekana wametuacha mbali kisa haya mabanda maana kila mtu kajenga anavyojua na kuezeka anavyojua. Dar inarudi kuwa Dar
Hizi akili za kibavicha hatari, sasa hujui ukimbimolea kesho atakuvamie akuibie hata kandambili nyumbani kwako
 
🔔Watafutiwe sehemu kwani wao ni akina nani?

🔔Wale vijana wenzao vijijini wanatafutiwa mashamba ya kulima na nani?

🔔Wale waliomaliza vyuo na shule mbalimbali wanatafutiwa kazi na nani?

🔔Kuna watu wana mamitji makubwa hawataki kukodi frem ati wao ni machinga watfutiwe eneo

🔔 Utaratibu wa mipango mji uheshmiwe na kila anayekuja mjini ajue anakuja kuishi vipi na sio kuanza kulalamika na kujiona wao ni kundi flani vulnerable ambalo linahitaji kutokufuata sheria lihurumiwe na kila mtu na liwe mzigo kwa serikali enyi WAMACHINGA na BODADODA ninyi ni akina nani?
 
Wenye nguvu ya fedha washafanya Yao tena,

Ndiyo tunajua, kila kitu lazima kiende Kwa utaratibu, Labda niulize Kwa Mleta uzi, Je Hilo gari linalotangaza halisemi mbadala wa hao wenye vibanda wanapaswa wapelekwe wapi?

Kama ndivyo, tayari hili ni kosa lingine kubwa baada ya lile la Kwanza la makampuni ya kigeni yanayokuja kuwekeza nchini hayatakiwi kuwekewa limiti ya wafanyakazi wanaotakiwa kuja nao kutoka makwao ili kufanya kazi kwenye kampuni hizo za kigeni!!

Hilo ndilo kosa kubwa kuliko mengine yote ambayo yameendelea kuwepo Wakati huu,

Watanzania mtegemee kukosa ajira kwenye makampuni yote ya kigeni na hata ysliyowekeza tayari mtaanza kutimuliwa mdogomdogo na wageni kuletwa kufanya kazi hizo

Yetu macho
Umewahi kufanya kazi katika kampuni za wahindi?. toka zamani wao wanaleta wahindi wenzao kufanya kazi hata ya ulinzi. Kuleta wafanyakazi haijaanza leo. je unafikiri watanzania hawana sifa, wavivu au hawaaminiki?
 
Wenye Mabanda yote kando ya barabara wametakiwa kuyabomoa kabla ya tarehe 18 mwezi huu ambapo ndio tarehe ya bomoabomoa. Mtakumbuka jinsi mabanda yayivyokua yameshamiri kila pande ya jiji na kuharibu kabisa muonekano wa mji kama miji minginge mikubwa ya majiran zetu hadi kufikia kuonekana jiji lote ni slum. Kuanzia maeneo ya fire,DIT hadi kisutu ilikua kituko hata kupishana watembea kwa miguu ni shida. Mlimani city ndio usiseme kabisa. Angalau jiji litaanza kuonekana sasa maana moshi wa mamantilie wanaopikia kuni pembeni ya barabara ndo ulikua unaonekana.Yaani hata Nairobi au Kigali tu walikua wanaonekana wametuacha mbali kisa haya mabanda maana kila mtu kajenga anavyojua na kuezeka anavyojua. Dar inarudi kuwa Dar
Hapo sasa ccm na maisha ya watanzania yataimarika sana..

Tutegemee chadema kuanza kutetea wamachinga?
 
Back
Top Bottom