Yote yamesababishwa na kufa kwa uchumi wa nchi.Mfano korosho, mbaazi, ufuta,mifugo bei ikiwa nzuri kilimo kikilipa nani awe machinga hali wanunuzi ukufuata shamba.
Kabla ya mwendazake Wakenya walijaa hadi vijijini wakichumbia mazao yaani unapewa advance mazao yakikomaa unamaliziwa cash yako wanavuna mazao yao we unabakia na pesa.Walijaa Mbeya,njombe,iringa, kilimanjaro kwenye ndizi,viazi mviringo,walijaa dodoma iringa rukwa ruvuma kwenye mahindi walijaa pwani tanga kwenye matikitiki,nyanya,mboga nk.Huku wabongo,wazambia wakijaa kanda ya ziwa hadi visiwani wakinunua dagaa, samaki,mabondo, Wacomoro, zimbabwe, zambia wakijaa kariakoo kuleta pesa hii ilisaidia Sana watu kubakia sehemu moja kuzalisha.Baada ya sera chakavu za kuwafanya matajiri wawe masikini,na kufunga mipaka,bifu zisizo kichwa majirani zetu wote walipotea hali ikawa ngumu vijijini ikapelekea wimbi la machinga mijini.
Tukivutia Wawekezaji ajira zitakuwepo,tukifungua mipaka wakulima na wafugaji watauza nje uzalishaji utarejea na idadi ya machinga itapungua mijini.