Vibanda vilivyowekwa kando ya barabara Jijini Dar es Salaam kuondolewa

Vibanda vilivyowekwa kando ya barabara Jijini Dar es Salaam kuondolewa

Wenye Mabanda yote kando ya barabara wametakiwa kuyabomoa kabla ya tarehe 18 mwezi huu ambapo ndio tarehe ya bomoabomoa. Mtakumbuka jinsi mabanda yayivyokua yameshamiri kila pande ya jiji na kuharibu kabisa muonekano wa mji kama miji minginge mikubwa ya majiran zetu hadi kufikia kuonekana jiji lote ni slum. Kuanzia maeneo ya fire,DIT hadi kisutu ilikua kituko hata kupishana watembea kwa miguu ni shida. Mlimani city ndio usiseme kabisa. Angalau jiji litaanza kuonekana sasa maana moshi wa mamantilie wanaopikia kuni pembeni ya barabara ndo ulikua unaonekana.Yaani hata Nairobi au Kigali tu walikua wanaonekana wametuacha mbali kisa haya mabanda maana kila mtu kajenga anavyojua na kuezeka anavyojua. Dar inarudi kuwa Dar
 
Kama pale ilala boma kutokea kigogo mwisho ni kero tupu!wamehodhi eneo lote lile,soko la mchikichini kulikua na parking kubwa tu upande breweries lakini sasa hivi vimejaa vibanda hamna parking tena!
 
Uchumi wa nchi hauwezi inuliwa na machinga bali kwa uzalishaji.
Machinga na bodaboda ni madalali wa viwanda vya china kukuza uchumi wa China

Zinaheshimika biashara za machinga. Wenye maduka na biashara kubwa walikuwa wahanga wa TRA. Uchumi gani unajengwa na wamachinga??? Hawa wapangiwe maeneo maalumu. Sio kila eneo ni la kufanya biashara. Mji uwe safi na wao waishi kama wananchi wa Tanzania.
Tukiwa hatufuati sheria na taratibu tujue tunajukomoa wenyewe
 
Yaani ilikuwa fululu-fululu.
Wenye Mabanda yote kando ya barabara wametakiwa kuyabomoa kabla ya tarehe 18 mwezi huu ambapo ndio tarehe ya bomoabomoa. Mtakumbuka jinsi mabanda yayivyokua yameshamiri kila pande ya jiji na kuharibu kabisa muonekano wa mji kama miji minginge mikubwa ya majiran zetu hadi kufikia kuonekana jiji lote ni slum. Kuanzia maeneo ya fire,DIT hadi kisutu ilikua kituko hata kupishana watembea kwa miguu ni shida. Mlimani city ndio usiseme kabisa. Angalau jiji litaanza kuonekana sasa maana moshi wa mamantilie wanaopikia kuni pembeni ya barabara ndo ulikua unaonekana.Yaani hata Nairobi au Kigali tu walikua wanaonekana wametuacha mbali kisa haya mabanda maana kila mtu kajenga anavyojua na kuezeka anavyojua. Dar inarudi kuwa Dar
 
Yaani wametubanaaje!!! Tunakoswa koswa na magari utadhani hatuna haki kutembea pembeni maana wamejaa wao. Halafu ole wako ukanyage kitu cha mtu!!!!
Ukikanya bahati mbaya wanakukoromea,na kukutishia watakuitia mwizi ili wakushambulie,ni kweli inapaswa waondoke sasa,maana ni sehemu ya wapita kwa miguu!!
 
Gari la tangazo linapita kutangaza ya kuwa ifikapo tarehe 18 mwezi huu hakitakiwi kibanda chochote kuonekana kando kando ya barabara katika jiji la Dar es salaam.

20210503_065320.jpg
 
Back
Top Bottom