Vibarua viwandani au part time job kwa hapa Dar es Salaam zinapatikana wapi?

Asante Sana umenena vyema haya ndio mawazo ambayo alietoa unajua kabsa amewah au ndo yupo kwenye gari moja nawewe
Kabisa bro tupo behewa moja (graduate 2017) na ajira rasmi bado, mimi ajira naiona ni moja ya vyanzo vingi vya mapato. Kama ajira bado basi vipo vyanzo vingine vingi vya mapato (Fursa) mbalimbali. Ni kujipanga, kufanya research za fursa mbali mbali na kuanza fursa.
 
"Mtaji Mtaji Mtaji"

Nimemnukuu graduate mmoja hapa makumbusho.
Mtaji mkubwa kabisa ni 1. Akili 2. Nguvu zako 3. Mdomo. Kama unayo mitaji hii basi unaweza kujipanga na kutengeneza mtaji pesa. Kivipi? Unaweza kutumia mtaji wa akili, nguvu na mdomo ukajiwekea malengo ya miezi kadhaaa ukafanya udalali wa vitu vinavyouzwa kama nyumba, magari, kiwanja n.k Ukapata mtaji pesa, Katika huo mtaji pesa utaopata unajiwekea malengo, mwisho wa siku utapata mtaji pesa wa kutosha kuanza project yoyote. Kikubwa malengo+nidhamu ya pesa+uvumilivu
 
Unahakika kuwa wewe si keyboard worrior??
 
Nikikumbuka waliofanikiwa kuendelea na shule walivyoniacha mtaani kwa mbwembwe na dharau najikuta sihisi chochote nikisikia msomi analia
 
Tatizo siku hizi vijana mnachagua sana kazi. Kama huna kazi ni ngumu sana kupata kazi namaanisha mchongo wa kazi halali hata kama ni kusaidia fundi ndio unaondoa gundu ndio mwanzo wa safari
 
Mungu anamuona anayepambana, nakumbuka nimefanya kazi zote za hovyo nikiwa mtaani

Mungu akaniletea ajira miguuni mwangu

Wala sikuwa na connection yoyote na mpaka leo sina mtu mkubwa nayefahamiana naye serikalini
M

Mungu asaidie dunia kwakweli.
 
hakika hakika💯%
 
Mimi ni kijana wa miaka 17 nikiwa na Elimu ya chuo kikuu shahada ya uhandisi wa mitandao na mitambo! Naomba kutumika Kama msaidizi Kwa kutumwa kazi mbalimbali maana najua watu wengi wako bize na Mambo ya kiofisi hata kushindwa kupata muda wa kufanya au kusimamia vitu vingne. Nipo tayari kutumwa popote Kwa mskubaliano maalumu ya malipo.
Nina ujuzi wa udereva pia na leseni na uzoefu wa kuendesha magari Kwa zaidi ya miaka 5 hapa Dar es salaam!
Nitume popote pia nafanya typing Kwa haraka na ishu zoote za stationary hivyo Kwa mahitaji hayo tuwasiliane Kwa namba 0776662470
 
Duh! Umenikumbusha mbali Sana Mkuu, maisha haya ya vibarua yalinitesa Sana, nakumbuka Kama ilivyokuwa kawaida yangu kuamka Alfajiri ya saa kumi na moja Alfajiri ili niwahi kupon ya kuingia kiwanda Cha kutengeneza nondo pale vertinary, Mzee Mohammed ndio ilikuwa kazi yake kugawa kupon, utakuta Ana kupon 20 halafu tunaotaka kazi tupo 50! Kwa kweli ni huzuni kuu, ataanza kuangalia anaowafahamu Kwanza.
Nilibahatika kupata kupon Mara Tatu tu lakini nilikua natimba pale kwa karibu Kila siku.
Ila Mungu ni mwema Kaka usikate tamaa, pambana! Tambua ww ni mshindi.
 
Ugumu wa maisha ulianza pale wasomi walipokuwa hawaajiliwi,wasomi wakawa wanalundikana na kuingilia biashara ambzo walipaswa kufunya wasio na elimu...sasa kama wasomi na wasiosoma wanafanya biashara moja je nani atakuwa mteja. Tuombe Mungu mama etu aangalie kwny swala la ajira namin Kila kitu kitakuwa sawa chochote utachouza kitakuwa na mteja.
 
Dahh.. Njia ni ngumu mno...Ila iko siku kaka hayo yote yatabaki kuwa story..! Usikate Tamaa.
 
Ila tuseme ukweli makonda wanamake aise...je ulifanikiwa kuzikusanya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…