Vichekesho vya Afrika: Waislamu wote wanadai Iran itashinda, Wakristo wanadai Israel itashinda.

Ponjoro wa Kinondoni

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2024
Posts
3,771
Reaction score
10,311
Wa Afrika mmerogwa na nani? Mmeshindwa kubaini wasio julikana wanaowateka na kuwaangamiza ndugu zenu mnakaa kusimuliana hekaya ambazo hata haziwahusu.

Kama haitoshi miaka nenda rudi ndugu zenu wa Congo wanaishi kama digidigi lakini hakuna anayejali. Natamani kuwaita kenge weusi nyie sema JF hairuhusu kutweza utu wenu.

Pole sana Africa. Waarabu na Wazungu wameharibu kabisa uwezo wa Mwafrika. Unakuta mtu yuko Buza anajifanya mzayuni damu, mwingine yuko kwa Mparange anajiona yeye ni mwajemi wa Iran. Pumbavu zenu nyie.
 
Asilimia 21 ya Waisraeli ni Waislamu
Wakristo ni asilimia 5.
Ni kosa la jinai Israel kujaribu kumtoa mtu Uyahudi kuwa Mkristo.
 
Tunaoabudu katika Hinduism, Paganism, Buddhism, Rastafarians , na hata Atheists tutembee vifua mbele kwani si Israel wala Iran itatuletea pesa kila siku maishani...🙎

Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.
 
Pole sana Africa. Waarabu na Wazungu wameharibu kabisa uwezo wa Mwafrika. Unakuta mtu yuko Buza anajifanya mzayuni damu, mwingine yuko kwa Mparange anajiona yeye ni mwajemi wa Iran. Pumbavu zenu nyie
Kwa nini uende kote huko mbali, wakati vita yetu wenyewe tayari tunayo ha a hapa; au hujui kinachoendelea sasa hivi?
 
Suala la Uzayuni siyo suala la dini wala kabila. Ni suala la nchi (Palestina) kuvamiwa na kukaliwa kinyume cha sheria ya kimataifa na maazimio ya UN. Ni sawa naa Ukaburu wa Afrikaa Kusini ulivyolaaniwa na wanadamu wote wa dini zote na kabila zote
Ndio maana nchi 170 duniani zinawaunga mkono Wapalestina. Mamilioni ya Wakristo na Wayahudi wanaunga mkono uhuru wa Palestina - HUU NI UKWELI HATA USIPOKUBALI
 
Anayesababisha vita pale ni mti mkavu ,kuna tetesi kavuta ..Nyie waafrika mnapigana kwa ujinga wa demokrasia. labda uniambie wapi nchi ya kifalme hapa Africa ikawa na civil war.

Unaongelea vita ya nje kufuatilia ,wakati mnatumia demokrasia iliyotoka Marekani .
 
Mbona unatulisha maneno Wakristo dhidi ya uovu wa Uyahudi na Marekani.
Ni vema kujua katika macho ya nyama Israeli ni nchi tu ipo pale ME.Na kiroho Israeli ni wale wote wanaomkiri Yesu Kristo kama bwana na mwokozi wa maisha yetu...Hii ndo Israeli ambayo haipigwi konzi.Hayo mengine ni ushirikana.Hivyo ushindi wetu tayari tulikwisha upata pale msalabani....vita yetu si juu ya damu na nyama.
 
Wa Afrika mmerogwa na nani? Mmeshindwa kubaini wasio julikana wanaowateka na kuwaangamiza ndugu zenu mnakaa kusimuliana hekaya ambazo hata haziwahusu.

Kama haitoshi miaka nenda rudi ndugu zenu wa Congo wanaishi kama digidigi lakini hakuna anayejali. Natamani kuwaita kenge weusi nyie sema JF hairuhusu kutweza utu wenu.

Pole sana Africa. Waarabu na Wazungu wameharibu kabisa uwezo wa Mwafrika. Unakuta mtu yuko Buza anajifanya mzayuni damu, mwingine yuko kwa Mparange anajiona yeye ni mwajemi wa Iran. Pumbavu zenu nyie.
Wakristo na waislamu ni wapumbavu kwa asilimia 99
 
Wanekata tamaa hawapendi kuthubutu
 
Back
Top Bottom