Mkuu, kwani unadhani mimi siyajui haya?Suala la Uzayuni siyo suala la dini wala kabila. Ni suala la nchi (Palestina) kuvamiwa na kukaliwa kinyume cha sheria ya kimataifa na maazimio ya UN. Ni sawa naa Ukaburu wa Afrikaa Kusini ulivyolaaniwa na wanadamu wote wa dini zote na kabila zote
Ndio maana nchi 170 duniani zinawaunga mkono Wapalestina. Mamilioni ya Wakristo na Wayahudi wanaunga mkono uhuru wa Palestina - HUU NI UKWELI HATA USIPOKUBALI
Tazama mada ilivyowekwa hapa ili ijadiliwe; na uhalisia wa makundi yetu hapa yanavyojigawa, siyo katika misingi hiyo unayoisemea wewe (ambayo ni sahihi); lakini tunaichukulia kama makundi ya kiimani.
Na tunapofanya hivyo, tunajitambulisha ni upande upi unaotuhusu kwa sababu nasi ni sehemu ya upande huo.
Sasa wewe niambie hii ya hapa kwetu, hasa Genge hili la Samia na Kikwete na woote wanaotuimbia "AMANI, AMANI"; tukumbuke kulinda AMANI yetu, kwa gharama yoyote ile (hata kumwaga damu ya waTanzania) kuilinda hiyo AMANI (?); lakini kundi hilo na washirika wake hawataki kabisa kusikia chochote kuhusu "AMANI inayolindwa na HAKI"!
Wewe haya unayaelezea vipi mkuu 'Ban Barka'?
Kweli unaamini ni lazima tudumishe AMANI; kwa sababu tu ya kuhakikisha Samia Suluhu Hassan anaendelea kubaki madarakani hata kama waTanzania walinyimwa HAKI ya kumpigia kuru HURU na bila ya mizengwe?