Vichekesho vya Afrika: Waislamu wote wanadai Iran itashinda, Wakristo wanadai Israel itashinda.

Mkuu, kwani unadhani mimi siyajui haya?
Tazama mada ilivyowekwa hapa ili ijadiliwe; na uhalisia wa makundi yetu hapa yanavyojigawa, siyo katika misingi hiyo unayoisemea wewe (ambayo ni sahihi); lakini tunaichukulia kama makundi ya kiimani.
Na tunapofanya hivyo, tunajitambulisha ni upande upi unaotuhusu kwa sababu nasi ni sehemu ya upande huo.

Sasa wewe niambie hii ya hapa kwetu, hasa Genge hili la Samia na Kikwete na woote wanaotuimbia "AMANI, AMANI"; tukumbuke kulinda AMANI yetu, kwa gharama yoyote ile (hata kumwaga damu ya waTanzania) kuilinda hiyo AMANI (?); lakini kundi hilo na washirika wake hawataki kabisa kusikia chochote kuhusu "AMANI inayolindwa na HAKI"!

Wewe haya unayaelezea vipi mkuu 'Ban Barka'?

Kweli unaamini ni lazima tudumishe AMANI; kwa sababu tu ya kuhakikisha Samia Suluhu Hassan anaendelea kubaki madarakani hata kama waTanzania walinyimwa HAKI ya kumpigia kuru HURU na bila ya mizengwe?
 
Soma vizuri utaelewa nilichomaanisha.
Bahati nzuri, huwa sibahatishi. Nikisha soma mara moja mada kama hii sihitaji tena kusoma nielewe maudhui yake ni nini.
Sina shaka yoyote kuwa wewe mwenyewe ndiye hujui maana ya hayo maneno niliyotumia hapo kwa uangalifu mkubwa.
Kwa hiyo usikwepe jukumu la kuelewa jibu hilo linahusu nini!
 
Juz nikamsikia yule prof lubumbashi wa kenya nae kaingia laini.
 
Hilo nalo neno,tutalifanyia kazi.
 
Ponjoro naona kapasua yai Viza kazi kwenu waislaeli na waajemi wa nyamilembe.
 
Ufafanuzi mzuri na inatakiwa uwe na kiwango kikubwa cha akili ili uweze kuelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…