Video: Afande IGP Sirro anamjibu nani hapa?!

Video: Afande IGP Sirro anamjibu nani hapa?!

Polisi ni kazi ya heshima kuliko wanasiasa, iliyotukuka inayotambuliwa kikatiba kama ukitimiza wajibu wako kwa mujibu wa sheria na kutumia akili. Askari mwenye akili nzuri aweza kuwa mwanasiasa anayeheshimika baada ya kustaafu.
Katiba inamtaka polisi asipendelee chama chochote wala asioneshe mapenzi yake kwa chama fulani kwa uwazi.
Hata hivyo, kwa sababu tu ya ujinga, polisi wetu wanadhihirisha hadharani upendeleo kitu ambacho huwaudhi hata wale wanaopendelewa kama wana akili na mapenzi kwa taifa.

Mbowe alikuwa na Gari la KUB na dereva Kenya na alipoambiwa alirudishe maneno yake uliyasikia kipindi kile.

Hivyo na ieleweke kwa kila mtu Polisi na vyombo vya dola vingine ni Resources available kwa chama kinacho tawala na serikali yake kufanya nchi iongozeke.
 
Polisi na vyombo vya dola siyo kwa ajili ya chama bali taifa.

Wanatakiwa wawe tayari kufanya kazi na chama chochote (ustaarabu na akili nzuri).

Vyama vitapita lakini taifa litakuwepo. Ni muhimu kwa raia/mwananchi (citizen) aelewe kuwa pamoja na chama chake, wananchi ni wamoja na wanaunganishwa na taifa moja lililokuu kuliko vyama.

Vyombo vya dola ikiwemo polisi wanatakiwa kushirikiana kudhibiti viongozi wa vyama wanaovunja katiba ili kulinda taifa lisiparaganyike na kamwe wasishiriki kuvunja katiba.
 
View attachment 2160498

Najaribu kuwaza, hapa Afande IGP anamjibu nani? Nikifiria zaidi nahisi kama anamjibu mama.

Msikilize mama hapa 👇
View attachment 2160533

Kweli wanafanya kazi zao. Nenda karipoti simu imepotea uone cha moto.

Nenda kawaambie una madini unahitaji usalama wao. Nenda kawaambie kuna mkusanyiko wa wanachama wa vyama kinzani.

Nenda kawaambie watoa milioni 100 benki wahitaji usalama wao. Nenda kawaambie unatoa ripoti ya rushwa kwa mmoja wa askari mwenzao…
 
Nchi imejamba hii, kila mmoja na lwake, vururu vururu..!
 
Yote ni yote, ila sio heshima, kweli jeshi linafanya madudu, hivyo mkuu akae kimya? Mkuu pia anahitaji heshima, si kusema sema kwa kuzunguka zunguka, mwenyewe akitambua atajisiaje? Kama nafasi inakushinda unaaga kiustaarabu, ni kawaida, unaweza kujitahidi kurekebisha ila inashindikana, hivyo unaomba kupumzika!
 
Mama aache mipasho ya kwenye majukwaa. Anapaswa kujitambua kuwa yeye ndiye kiongozi mkuu wa nchi, na hivyo vyombo vyote anavyovipasha kwenye majukwaa ni vyake/viko chini yake. Kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi kwa vyombo hivyo ni ishara tosha ya kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi kwa anayevisimamia!
 
Sio kwa matakwa ya Katiba ya JMT?
Watu bado hawaelewi hili, Samia yupo hapo kwa roho nzuri walizoonyesha wakuu wa ulinzi wakati ule wa msiba.

Bila wao tayari alikuwa kapigwa bao.
 
Mimi nauliza wale wapuuzi wa CCM Kuna yoyote aliyeitisha press kumsema Sirro kama walivomshambulia Ndugai?

Sirro ameonesha uanaume, form 4 failure asiyejua mambo ya Nchi anasimama kwenye jukwaa anabishana na mtaalam.

Huyu kilaza anadhani Polisi wakiaamua kutofanya kazi kama miaka nyuma na kuacha Chadema waruhusiwe kuandama Chama chake kitaendelea kukaa hapo.

Fikiria Police waamue kuacha kuwasaidia CCM Kwenye vituo vya kuhesabia kura.

Yaani tumepata funzo never again Form 4 failure na mtu mwenye Elimu ya kuunga unga kuwa Rais
 
Sirro amekosa self awareness.

Swala sio polisi kuwakamata polisi wenzao.

Swala kubwa ni kwanini maofisa tena kwa kushirikiana kupanga na kutekeleza uhalifu.

Walifikaje kupewa vyeo vya kuongoza polisi kwenye wilaya ikiwa wana mienendo ya namna hivyo?

Je ni matukio mangapi ambayo hayakufika huku juu?

Mmoja wao ndio aliyemtolea silaha Waziri Nape hadharani, ilikuwaje akapewa kuongoza upelelezi wa Wilaya?

Askari asiye na nidhamu kiasi kile, alipitaje mchujo?
Inakuwaje maofisa hawaoni shida kukamata mtu na kumuua akiwa mikononi mwa jeshi la polisi? Afadhali hata kina Zombe

walitengeneza filamu ingawa iliwalipukia.

Anayechukiwa sio Sirro, jeshi zima linahitaji mabadiliko. Haliaminiki kabisa na wananchi.

Tumesikia vituko vingi kwenye kesi ya Mbowe, leo ukiwauliza wananchi kama stori za kina Adamoo zina ukweli ndani yake, nina uhakika majority watasema ni za kweli.
Acha kukariri aliyemtolea bastola nape hayupo hapo! Mitandao sio poa!
 
Mimi nauliza wale wapuuzi wa CCM Kuna yoyote aliyeitisha press kumsema Sirro kama walivomshambulia Ndugai?

Sirro ameonesha uanaume, form 4 failure asiyejua mambo ya Nchi anasimama kwenye jukwaa anabishana na mtaalam.

Huyu kilaza anadhani Polisi wakiaamua kutofanya kazi kama miaka nyuma na kuacha Chadema waruhusiwe kuandama Chama chake kitaendelea kukaa hapo.

Fikiria Police waamue kuacha kuwasaidia CCM Kwenye vituo vya kuhesabia kura.

Yaani tumepata funzo never again Form 4 failure na mtu mwenye Elimu ya kuunga unga kuwa Rais
Kama tulivyopata funzo ya kutorudia tena kumuweka mhutu kwenye kiti kile.
 
Ccm hawana shukrani pamoja na Kazi kubwa aliowatendea siro ya kuwapa ushindi wamemuwashia taa nyekundu.
 
bila kupiga kelele walikuwa wamejikausha! IGP alikuwa anafaham ila kwakuwa amezoea kuua basi akaona kawaida!

Kiukweli angepumzika tu maana zama za aina yake na matukio yaliyofanywa na Polisi awamu ya 5 ni maisha tofauti na awamu ya 6! kwa hiyo ajiongeze maana mama anataman aweke timu yake kama Mwendazake alivyoweka! SIRRO angestaafu kwa heshima tu

Mama aliachia mpaka ushahidi wa polisi kesi ya mbowe usikike mbele ya watanzania wote, aibu ile haiwezi jificha! mama kila akiwaona polisi anakereka!

Sirro apate wasaa akae na mama amuombe amsamehe mahali alipomkwaza aombe apumzike! mama muungwana sana maana mama ni mama
Nani alikuambia igp alikuwa anajua. Masshuuz jazz band😏😏
 
View attachment 2160498

Najaribu kuwaza, hapa Afande IGP anamjibu nani? Nikifiria zaidi nahisi kama anamjibu mama.

Msikilize mama hapa 👇
View attachment 2160533

Mama na Sirro hawaivi.
 
Back
Top Bottom