Video: Afande IGP Sirro anamjibu nani hapa?!

Video: Afande IGP Sirro anamjibu nani hapa?!

Mimi ni mtoto wa Polisi tena Baba na Mama ni wastaafu. Tatizo sio Polisi bali ni Polisi kujiingiza kwenye siasa . Chuki hii ndiyo inafanya watu waanze kutokuiamini na kuchukia Polisi. Hivyo wenye akili kama Mangu ambaye ali jaribu kufanya hili waliondolewa hawa ndiyo walikuwa wanajali idara ya Polisi.
Mangu alifanyaje
 
Hawajui askari huyo..hata issue ya mbowe kuachiwa imewaudhi baadhi.wanasema boss wao ni kama amedhalilishwa vile.
Wataondolewa...Si jeshi lipo na Wapo Wengi tuuu Tupo tayari kuajiriwa na kutenda Vizuri..Mara Mia..
 
Wapi ulishawahi ona Mwanamme kutoka kanda ya ziwa akiyumbishwa na mwanamke? Hapa ni bora busara itumike mama ajifunze kuwaheshimu wakuuu wa vyombo vya ulinzi na usalama maana ndio wamemuweka hapo.

Sasa tabia ya kuwasema katika speech zake haipendezi hata kidogo, mama ajitathimini hata kama yeye ni namba moja?

Alikuwepo boss wake JPM sasa hivi yu wapi? Aache jazba na ubabe hajiulizi why magufuli alikuwa akiwaweka karibu top three (3) halafu yeye anawapanda kichwani.

Siku hawa wakicharuka hata hapo jengo jeupe hapatakalika, ajifunze kuzungumza nao kwa uweledi.
Hakuna chakucharuka...Siro hawezi kumjibu Samia kama anamuongelesha muuza bar take huko Gongolamboto
 
Mangu alifanyaje
Kama kumbukumbu zangu ziko sawa kuna Amri ilitolewa na Mkuu Wa Mkoa Arusha wakati ule Gambo ya kuwakamata watu fulani (nimesahau kwa kosa gani)..

Lakini Mangu akawaagiza Vijana wake wapuuzie lile agizo la Mkuu Wa Mkoa na kwamba hayo ni mambo ya Kisiasa... Baada ya hapo haikupita Wiki Hayati akatengua Uteuzi wa Mangu kuwa IGP akamteua Balozi Malawi...

Kumbuka wakati huo Ziro alikuwa Chawa Wa Bashite, nadhani Bashi boy akampigia pande kwa Babake ndipo Ziro akapandishwa kuwa Aijipii
 
Naona 'kama huwezi amini chombo chako' imerudiwa hapa......ziroooooooooo.
 
acheni uchochezi,ila pale mwisho ukiandika habari ya maendeleo ya tumbaku hahahahaha,kumbe kamanda mcheshi sana ila naona huyu mleta mada hajaanzia mwanzo ili kugombanisha.
 
Acha kutetea upuuzi mkuu,ukosoaji hauwi vile unavyotaka wewe kiasi kwamba unaota vichambo sijui mioasho nk.

Afu Polisi hawajaanza leo kuzingua na watu kama sio wote hawana Imani na Polisi,hao polisi wamesimamia mauaji awamu iliyopita lazima wabadilishwe.
Zamani polisi walikua Hawaui?
 
Mfumo wa vyombo vya ulinzi na usalama kujibizana kwa mitandao kumlenga Amiri jeshi mkuu ni hatari sana kwa mkuu wa nchi.
CCM mliangalie kwa undani hilo.
Kabla ya kubadilisha polisi, CCM walitakiwa waanze kubadilishwa wao.
Kabisa unasema CCM waangalie hilo?
 
Kama kumbukumbu zangu ziko sawa kuna Amri ilitolewa na Mkuu Wa Mkoa Arusha wakati ule Gambo ya kuwakamata watu fulani (nimesahau kwa kosa gani)..

Lakini Mangu akawaagiza Vijana wake wapuuzie lile agizo la Mkuu Wa Mkoa na kwamba hayo ni mambo ya Kisiasa... Baada ya hapo haikupita Wiki Hayati akatengua Uteuzi wa Mangu kuwa IGP akamteua Balozi Malawi...

Kumbuka wakati huo Ziro alikuwa Chawa Wa Bashite, nadhani Bashi boy akampigia pande kwa Babake ndipo Ziro akapandishwa kuwa Aijipii
Umesema uongo, aliyekataa alikua RPC Shana. Ila pia kukataa huko hakuwezi kuwafanya polisi kuwa bora. Maana mbona huyohuyo RPC alikamatwa tena vijana wa chadema na lema
 
Umesema uongo, aliyekataa alikua RPC Shana. Ila pia kukataa huko hakuwezi kuwafanya polisi kuwa bora. Maana mbona huyohuyo RPC alikamatwa tena vijana wa chadema na lema
Yes tamko la kukataa lilitoka kwa RPC, lakini IGP ndiye alimwagiza RPC Asitekeleze Agizo la RC.. Na uteuzi Wa IGP ukatenguliwa kipindi hicho hicho...
 
Walivyomaliza mda wao hawakuongezewa,Siro amestaafu kitambo ni WA kupumzika.

Maofisa wa chini yao walishughulikiwa wakiwemo Abdallah Zombe nk.
Sirro ana miaka 58, muda wa kustaafu bado.

Achana na zombe mmoja, kuhusu kushughulikiwa jiwe mwenyewe aliwahi kuwashughulikia polisi 450 Uliona kilibadilika nn?
 
Back
Top Bottom