Video: Afande IGP Sirro anamjibu nani hapa?!

Video: Afande IGP Sirro anamjibu nani hapa?!

Nikisikiliza hotuba za Hangaya.

Nikisikiliza kauli za Sirro,
Nikikumbuka ya Ndugai.

Naona kama kuna njia panda nyingi huko juu.
 
Kuna vita kubwa sana kati ya vyombo vya ulinzi na usalama na namba moja, wote sasa hivi wanajutia kwanini walimbeba maana ya chumbani anaishia kuyaweka sebuleni…

Embu tujipe muda ila kwa ufupi mabadiliko ni muda wowote kwa baadhi ya viongozi hao…
TPDF naona hakuna m utano mkuu
 
Sirro amekosa self awareness.

Swala sio polisi kuwakamata polisi wenzao.

Swala kubwa ni kwanini maofisa tena kwa kushirikiana kupanga na kutekeleza uhalifu.

Walifikaje kupewa vyeo vya kuongoza polisi kwenye wilaya ikiwa wana mienendo ya namna hivyo?

Je ni matukio mangapi ambayo hayakufika huku juu?

Mmoja wao ndio aliyemtolea silaha Waziri Nape hadharani, ilikuwaje akapewa kuongoza upelelezi wa Wilaya?

Askari asiye na nidhamu kiasi kile, alipitaje mchujo?
Inakuwaje maofisa hawaoni shida kukamata mtu na kumuua akiwa mikononi mwa jeshi la polisi? Afadhali hata kina Zombe

walitengeneza filamu ingawa iliwalipukia.

Anayechukiwa sio Sirro, jeshi zima linahitaji mabadiliko. Haliaminiki kabisa na wananchi.

Tumesikia vituko vingi kwenye kesi ya Mbowe, leo ukiwauliza wananchi kama stori za kina Adamoo zina ukweli ndani yake, nina uhakika majority watasema ni za kweli.
 
Sijui ni kwa nini hadi sasa hivi huu uzi upo?

Hivi IGP Sirro ni wapi hapa amemjibu Mkuu wa nchi, Rais na Amiri Jeshi Mkuu?

Huu si uhuru wa maoni ni kosa kubwa sana kisheria hili. Wakuu wetu wa vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi hii ni watiifu na wazalendo mno.

Tuache hii tabia mbaya kabisa kuchonganisha viongozi wetu.🙏🙏🙏
 
View attachment 2160498

Najaribu kuwaza, hapa Afande IGP anamjibu nani? Nikifiria zaidi nahisi kama anamjibu mama.

Msikilize mama hapa 👇
View attachment 2160533


anasema nini huku bhooo bhoo bhoo,
 
Sijui ni kwa nini hadi sasa hivi huu uzi upo? Hivi IGP Sirro ni wapi hapa amemjibu Mkuu wa nchi, Rais na Amiri Jeshi Mkuu? Huu si uhuru wa maoni ni kosa kubwa sana kisheria hili. Wakuu wetu wa vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi hii ni watiifu na wazalendo mno. Tuache hii tabia mbaya kabisa kuchonganisha viongozi wetu.🙏🙏🙏
Unapata nini ukipotosha?

Mnakimbilia kufunika vitu badala kuvi solve, sasa uzi ufutwe kwa kipi
 
Sirro amekosa self awareness.

Swala sio polisi kuwakamata polisi wenzao.

Swala kubwa ni kwanini maofisa tena kwa kushirikiana kupanga na kutekeleza uhalifu.

Walifikaje kupewa vyeo vya kuongoza polisi kwenye wilaya ikiwa wana mienendo ya namna hivyo?
Je ni matukio mangapi ambayo hayakufika huku juu?
Mmoja wao ndio aliyemtolea silaha Waziri Nape hadharani, ilikuwaje akapewa kuongoza upelelezi wa Wilaya? Askari asiye na nidhamu kiasi kile, alipitaje mchujo?
Inakuwaje maofisa hawaoni shida kukamata mtu na kumuua akiwa mikononi mwa jeshi la polisi? Afadhali hata kina Zombe walitengeneza filamu ingawa iliwalipukia.

Anayechukiwa sio Sirro, jeshi zima linahitaji mabadiliko. Haliaminiki kabisa na wananchi. Tumesikia vituko vingi kwenye kesi ya Mbowe, leo ukiwauliza wananchi kama stori za kina Adamoo zina ukweli ndani yake, nina uhakika majority watasema ni za kweli.
Askari aliyemtolea nape bastola sio mmoja ya hao wa mtwara. Sijui nani kawamesesha hili,
 
Sijui ni kwa nini hadi sasa hivi huu uzi upo? Hivi IGP Sirro ni wapi hapa amemjibu Mkuu wa nchi, Rais na Amiri Jeshi Mkuu? Huu si uhuru wa maoni ni kosa kubwa sana kisheria hili. Wakuu wetu wa vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi hii ni watiifu na wazalendo mno. Tuache hii tabia mbaya kabisa kuchonganisha viongozi wetu.🙏🙏🙏
aliyesema ...unakwenda kujibiwa bhooo bhoo ni sisi? 🤣🤣🤣🤣🤣
 
Askari aliyemtolea nape bastola sio mmoja ya hao wa mtwara. Sijui nani kawamesesha hili,
1647980553152.png
 
CCM bila ya nguvu ya Polisi sijui itakuwaje? IGP hawezi mjibu Amiri Jeshi Mkuu hata siku moja. Anatoa maoni yake kuwapelekea ujumbe wale waliotoa maoni yao ndani ya kikao cha CCM kuhusu Polisi na yakatangazwa na Mwenezi wa CCM hadharani. Haikuwa njia nzuri sana ya kuwa adress wadau muhimu kwa CCM kama Polisi.

Na IGP kasema wazi usishambulie Polisi kama Polisi. Lakini waweza kumshambulia IGP utakavyo maana yeye ni rahisi tu ukiamua unamnyanganya nafasi hiyo unaweka mtu wako mwengine unaye endana naye. Lakini ukilishambulia jeshi zima kwa sababu tu ya IGP ni hatari kubwa. Na ndio ukweli wenyewe maana philosophy ya vita kwa majeshi yote ni hii, an injury to one is an injury to all.
Polisi ni kazi ya heshima kuliko wanasiasa, iliyotukuka inayotambuliwa kikatiba kama ukitimiza wajibu wako kwa mujibu wa sheria na kutumia akili.

Askari mwenye akili nzuri aweza kuwa mwanasiasa anayeheshimika baada ya kustaafu.


Katiba inamtaka polisi asipendelee chama chochote wala asioneshe mapenzi yake kwa chama fulani kwa uwazi.


Hata hivyo, kwa sababu tu ya ujinga, polisi wetu wanadhihirisha hadharani upendeleo kitu ambacho huwaudhi hata wale wanaopendelewa kama wana akili na mapenzi kwa taifa.
 
Back
Top Bottom