I agree
Lakini muda mwingine tutenganishe siasa na changamoto za maisha ya kila siku.
Imani na jeshi la polisi ni kitu muhimu sana katika kupambana na uhalifu, ni kukosa imani na polisi ndio kilichopelekea kijana aliechukuliwa mbele ya mashahidi luluki halafu wote waamue kubaki kimya; na ingebaki ivyo kama baba yake mzazi asingepaza sauti.
Ni kitu gani kilichowaogopesha vijana wote aliokuwa nao marehemu bar siku anakuja kubebwa na polisi waogope kupaza sauti baada ya kuto muona siku kadhaa.
Sasa mambo kama haya embu tutenge kidogo siasa nakujiuliza ni namna gani tunaweza toa habari kama hizi bila ya woga huko juu waanze kufuatilia; katika harakati za kuboresha ujirani mwema na hii taasisi maana ni muhimu katika maisha yetu wao wakiwa kama walinzi wa mali na maisha kwenye jamii.