Video: Afande IGP Sirro anamjibu nani hapa?!

Siro alikuwa anajitetea.Pili kama muundo wa Polisi una shida urekebishwe afu ikitokea matukio kama haya Ma RPC wawe wanaondolewa fasta kwa kuletwa Makao makuu au kupangiwa majukumu mengine.
 
Hizi akili huwa mnatoa wapi? Kwenye tukio la Lissu unaitenganishaje Polisi na CCM?

Kwamba Siro aliamua tu mwenyewe (ikiwa ni yeye) kwenda kumshambulia Lissu? Hiyo hata Samia hawezi kuifufua.

Hahaha vita ya CCM kwa CCM haiwezi kuwanufaisha CDM hata siku moja, nyinyi mnachotakiwa kufanya ni kutafuta namna ya kuingia kwenye system.
 
Sirro aweza kuwa mpuuzi kwa kiwango fulani,ila hazuii nia nzuri ya maslahi bora kwa askari kama ipo kwa huyo rais wake.

Sirro amezungumza kama mwenye taaluma ya polisi chombo anachokiongoza,kwamba kama shida anayo yeye,apigwe yeye kwa namna yote.ila kuinyea taasisi nzima sio jambo salama.

Embu nieleze hao maofisa bora si wako kazini saa hii wakiugulia maumivu ya vichambo kama polisi wengine wasio waadilifu???
 
Siro alikuwa anajitetea.Pili kama muundo wa Polisi una shida urekebishwe afu ikitokea matukio kama haya Ma RPC wawe wanaondolewa fasta kwa kuletwa Makao makuu au kupangiwa majukumu mengine.
Na ndio maana sijamlaumu IGP moja kwa moja kwa sababu alipopata habari alishugulikia akaondoa chain nzima ya wahusika.

Lakini tumefikaje hapo hadi ndugu walalamike mitandaoni ndio IGP ajue. Issue ya msingi inaonekana wananchi hawana imani na jeshi la polisi kwenye kuripoti matukio ya uhalifu wa polisi na ndicho alichoongea raisi pia.

Ndio maana kwenye post ya kwanza uliyo quote nikatoa suggestion either namba ya kuripoti uhalifu iwe independent na polisi; au kuwe na number maalum wizara ya mambo ya ndani ya kuripoti matukio ya uhalifu wa polisi ili waziri na IGP wawe briefed mapema to take actions.
 
Kuna tatizo ktk mfumo wa kikazi (operations) katika jeshi la Polisi.



Haiwezekani mtu anaingia Polisi Station/ Polisi Post huku kasindikizwa na mtu, halafu apotelee ndani ya kituo cha Polisi, ni upungufu kubwa ktk mfumo wa Polisi habari imfikie IGP kuwa mtu huyo aliyekamatwa na jeshi la Polisi akaingia kituoni kuwa akuuawa na askari wa jeshi la Polisi miezi miwili baadaye.

Kesi tajwa aliyoitaja IGP ya Mtwara ni kielelezo tosha cha mfumo mbovu uliopo ndani ya jeshi lisilofuata PGO, haki ya mtuhumiwa kuongea na mlinda amani / wakili au ofisa wa Mahakama n.k
CASE STUDY 1: Mtwara: Mfanyabiashara madini: auawa
Inatakiwa mtu akiingizwa ndani ya kituo chochote cha Polisi basi uhai wake uhakikishiwe pia hata mtuhumiwa akikamatwa nje ya kituo cha Polisi pia mfumo wa jeshi lazima unakili mara moja ktk mfumo wake kuwa kuna mtu amekamatwa. Hii itazuia jambo lolote lisilotarajiwa ktk utaratibu rasmi (wa PGO) kutotokea au mianya ya rushwa kuwepo, mahabusu / watuhumiwa kufichwa, kunyimwa haki ya dhamana n.k n.k

Sasa Ofisi ya makao makuu ya Polisi taifa pia Ofisi ya IGP inapaswa kuweka mfumo thabiti utaofuatilia na kunakili (ku register) ukamataji nje ya kituo cha Polisi au ktk kituo cha Polisi na kutekeleza kazi kwa kufuata PGO na kuhusisha wajumbe wa nyumba kumi kumi na wana familia kuhusu kuwa mtu ktk eneo lao au makazi amekamatwa na Jeshi la Polisi .

CASE STUDY 2:
Vijana wakamatwa na Polisi eneo la Kariakoo Dar es Salaam,; Familia zalia wametoweka mikononi mwa Polisi, hawajui tuhuma zao wala walipo


TAHARUKI: Familia zilizopotelewa na ndugu zao watano katika mazingira ya kutatanisha tangu Desemba 26, 2021 maeneo ya Kariakoo ‘Kamata’ wamepanga kuonana na Waziri wa Mambo ya Ndani awasaidie.

Kwa mujibu wa familia hizo, wamefikia hatua hiyo baada ya kushindwa kupata msaada kutoka kwa Jeshi la Polisi tangu waliporipoti jambo hilo Desemba 27, 2021. Soma zaidi:
 
Acha kutetea upuuzi mkuu,ukosoaji hauwi vile unavyotaka wewe kiasi kwamba unaota vichambo sijui mioasho nk.

Afu Polisi hawajaanza leo kuzingua na watu kama sio wote hawana Imani na Polisi,hao polisi wamesimamia mauaji awamu iliyopita lazima wabadilishwe.
 
Aigipii anazifuata nyao za yule spika aliye sahaulika kwa bidii! Bado press mbili tu, ya kuomba msamaha, (“nimekosa mimi!”) na kung’atuka!
 
Chawa wa mama hawezi kukuelewa
[emoji23][emoji23]

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
 
Jana chui jike nae alisema akiwalalamikia police wanamjibu tu kuwa mbona hana imani na vyombo vyake vya usalama,Takukuru nao wakisemwa wananuna.
Nchi ngumu sana hii.
Mama aendee Kwa step wanaweza kuzira kufanya naye Kazi ikawa shuuli kwel
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…