VIDEO: Askari Polisi alalamikia mishahara midogo

VIDEO: Askari Polisi alalamikia mishahara midogo

Kuna mwanadarasa wangu ameanza yupo na upolisi miaka 12 sasa, bado ni PC wakati walimu aliosoma nao darasa moja na wako kazini miaka 10 wote kwa sasa ni walimu wakuu. Elimu zao waote ni diploma, askari n dip ya uongizi na utawala.
 
Polisi wajinga sana, wanaona hiyo 460+300+rushwa=1200 kuwa wameyaweza maisha.

Tena wasote kabisa milele yote.
 
Huyo askari mwanaume wangemstaafisha tu yaani miaka 27 ya kufanya kazi bado hana hata nyota ni sergent tu looo uvivu wa kusoma .Huyu anatakiwa aondolewe cheo hicho ni cha vijana wadogo tu zee zima sergent !!! Haoni aibu?
Hana cheti cha F4
 
Kwani mishahara ya askar Bei GANI?

Samahan KWA swali wadau
 
Hawa wajitetee wenyewe mbuzi wa kafara hawa
 
Sasa mbona askar wa jwtz vijana wadogo wana nyota au V, tofaut na polis kumkuta kija ana nyota 3 au 2 ni nadra sanaa
Kupata nyota sio ukaaji wako muda mrefu kazini. Ukiona kijana kapata nyota ujue ana elimu ya kuanzia form six, na ameenda kozi za kiuafsa. Hata jeshini kuna wazee wengi tu wameishia vyeo vya mikononi, cheo cha mabegani vinahitaji elimu.
Na hao unawasema vijana wengi wa JWTZ wa miaka hii wameenda wakiwa na Elimu zao ndio maana. Sasa huo mzee ukute alienda police akiwa na form four, hawezi kwenda kusoma kozi ya uafisa ni hadi kwanza ajiendeleze kielimu kwanza.
Afu naona pia Police kozi za uafisa ni shida kuna mshikaji wangu ameingia police toka 2013 akajiendeleza kamaliza chuo mwaka 2018 hajapata kozi hadi saizi
 
Huyo askari mwanaume wangemstaafisha tu yaani miaka 27 ya kufanya kazi bado hana hata nyota ni sergent tu looo uvivu wa kusoma .Huyu anatakiwa aondolewe cheo hicho ni cha vijana wadogo tu zee zima sergent !!! Haoni aibu?
Mmesha watumia sasa mnawadharau. Uchaguzi ukifika mnawatukuza sana...
 
Huyo askari mwanaume wangemstaafisha tu yaani miaka 27 ya kufanya kazi bado hana hata nyota ni sergent tu looo uvivu wa kusoma .Huyu anatakiwa aondolewe cheo hicho ni cha vijana wadogo tu zee zima sergent !!! Haoni aibu?
Jamani tuwe wakweli katika hili. Wapo vijana wamehitimu form Six na kila waombapo kwenda kusoma wanakutana na kizingiti. Huyu kamaliza form four na ana miaka 27 kazini na ni Sergeant. Alianza kama Private, akapanda kuwa Lancecoplo, akapanda kuwa Coplo na baadae akapanda kuwa Sergeant na iwapo atajaliwa anaweza kupanda na kuwa Sergeant Major. Muundo wa polisi upo hivyo. Na katika kila cheo unatakiwa utumikie kwa kipindi fulani. Kumbuka pia hawa ni NCO, Non-Commissioned Officer, na wengi wao hustaafu wakiwa na cheo cha Sergeant, ni wachache ambao hupanda na kuwa Commissioned Officers. Huyu halalamikii kutokuwa na cheo. Anacholalamikia ni mishahara duni kulinganisha na wenzao katika sehemu nyingine ambao wote elimu yao inalingana.
 
Afande huyu lazima watamtafuta kimya kimya, awe makini sana.......
 
Ukiwa haujui jishushe ili ufundishwe ,JWTZ bila kuwa na degree/ACSEE na ukahitimu kozi ya chuo cha uafisa utaishia cheo cha mwisho WOI Wakati huo huo nimeshuhudia kwenye jeshi ka magereza kuna kamishna aliishia form four na pia askari wanatoka cheo cha Staff Sergeant mpaka moja kwa moja nyota moja na wanaambiwa chagua kuwa Sajini meja au kuwa Afisa

Magereza au polisi wapo wanaovaa nyota wakiwa na zaidi ya miaka 45+ ,kaulizie JWTZ kama unaweza vaa nyota una miaka kuanzia 36
TPDF unaweza kuwa Liutenant hadi ukiwa na miaka 22 ,kuna ambao wamewahi kuvaa na umri huo kwa kuwa na elimu ...lakini siku hizi kwakua kuna ushindani sana wa nafasi kuna ambao wanapata na miaka 25 ..ukienda vizuri miaka 36 ni umri wa kuwa Major au pengine captain kama umeenda taratibu na kuzembea kufanya mitihani ya kwenda course ...ukienda majeshi yote angalau ni TPDF tu ndio inajulikana ufanye nini upande ....ni wachache sana wana fluke na kupanda kwa upendeleo wanahesabika na huwa wanazomewa sana .,hawapewi heshima
 
Huyo askari mwanaume wangemstaafisha tu yaani miaka 27 ya kufanya kazi bado hana hata nyota ni sergent tu looo uvivu wa kusoma .Huyu anatakiwa aondolewe cheo hicho ni cha vijana wadogo tu zee zima sergent !!! Haoni aibu?
Nimewaza mbali sana zaidi yako.Angekuwa ndio mzazi wako ungesgauri hivi
 
Back
Top Bottom