VIDEO: Askari Polisi alalamikia mishahara midogo

mkuu ungekomaa na mabo ya vyama basi sana ccm ingekua safi sana.

haipendezi kujadili mambo ya kada sisiyo yako kwa mtindo wa ujuaji kiasi hiki.

wewe unadhani kila mwenye sifa anapandishwa cheo??mbona hapo lumumba wengi mnajipendekeza sana ili wenye uwezo wasisikike!!hizi ajira zenu zisizo za kuzalisha haziangalii potential ya mtu kazini,ila ni kwa namna gani ni chawa wa kiongozi.

kama umefatilia ziara ya mh rais udinduzi wa mabweni ya polisi,kuna askari alipata nafasi ya kutoa neno mbele ya mh rais,kwa jinsi alivyoongea tegemea apande vyeo sana na atasifiwa.sababu aliwasafisha wenyewe mbwa mbele ya rais.lakini huyu mzee hata kwa kumtizama usoni anaonekana sio wa kuchekea usen&,basi anasiginiwa kunguni.
 
hilo ni tatizo dunia nzima.

maana mkate ni mdogo wahitaji ni wengi.
jwtz kuvaa nyota ya kwanza mpaka 2 ni kazi nyepesi,shida inaanzia nyota ya 3.

halafu siku hizi askari kibao wa jwtz wanajiendeleza kielimu pia,hivyo jeshi huwapa kipaumbele hao zikitoka nafasi za cheo.
 
Afande huyu lazima watamtafuta kimya kimya, awe makini sana.......
wakati kawataka na wakubwa zake wa hightable kwamba nao wana mshahara sungura[emoji28][emoji28][emoji28].

labda wawe wamerogwa kama alivyosema.vinginevyo wanatakiwa wamshukuru tu.
 
sasa siku hizi wanapandisha vyeo kuanzia captain kwenda juu kwa kuangalia elimu ya kijeshi ...sio ya huku uraiani ..ni watu wachache tu kama Mbuge waliopata vyeo kwa matakwa ya mtu au kwa kupiga matofali ...hao askari wa vipaji waliisha kipindi cha Kiaro na MUSUGURI wale walikuwa na vipaji na uwezo mkubwa sana wa elimu ya kijeshi [field ]
 
Inasikitisha sana...Hawa ndio wanaolinda usalama wa raia na mali zao halafu wana njaa unategemea nini fisi kumkabidhi "BUCHA".
 
ndio maana askari wanasoma sana.

maana ipo mifano ya askari kadhaa wakivaa umajor moja kwa moja sababu ya elimu kubwa.

lakini hatuwezi beza ujuzi na uzoefu wa kijeshi kabisa,maana field hakutaki lecture.
watu wasisahaulike vyeo kisa hawajasoma elimu za degree.
 
Kwa kweli Polisi wana mishahara midogo sana.
Serikali inabidi wawafikirie wanausalama wote ili ingalau wafanye kazi kwa weledi na si kutegemea virushwa rushwa vya hvyo mitaani.
 
JWTZ mfumo ndio mgumu sasa maana kutokea askari kupata nyota lazima uende Chuo cha uafisa wakati Polisi,Magereza,Uhamiaji kutokea uaskari unaweza ukapewa tu nyota na mkuu wa jeshi eg IGP au CGP etc
JWTZ moto wa kuotea mbali.
Hata kama una vyeti akini cheo unahenyea, ndio maana tuna jeshi zuri sana kiutendaji.
Tunaona Nigeria wanavyohenyeshwa na Boko Haram, mfano wa Kbiti ni ushahidi tosha juu ya umahiri wa Jeshi letu.
 
JWTZ mfumo ndio mgumu sasa maana kutokea askari kupata nyota lazima uende Chuo cha uafisa wakati Polisi,Magereza,Uhamiaji kutokea uaskari unaweza ukapewa tu nyota na mkuu wa jeshi eg IGP au CGP etc
Kafanye homework yako vzr mazee hamna kitu kama hichi ulichokiandika
 

Ukishafikisha umri wa miaka kuanzia 36 umeshakosa sifa za kuwa afisa candidate na nyota unaisikia kwenye bomba tu mpaka milele labda Rais akupandishe kitu ambacho ni ndoto huwa haitokei

Wakati majeshi ya wizara ya mambo ya ndani wapo watu wanavaa nyota ya kwanza ana umri wa miaka zaidi ya 45 kitu ambacho Jeshini hakitokeagi na hakipo
 
Kafanye homework yako vzr mazee hamna kitu kama hichi ulichokiandika

Kuna mwanamke kapewa nyota moja jeshi la polisi kutokea uaskari sio muda mrefu sana kama unahitaji jina naweza kukutafutia nikipata muda, na sababu aliyopewa nyota ni alienda masomo Marekani akaandika thesis ambayo ilikuwa inatoa suggestion fulani kwa jeshi la polisi
 
JWTZ moto wa kuotea mbali.
Hata kama una vyeti akini cheo unahenyea, ndio maana tuna jeshi zuri sana kiutendaji.
Tunaona Nigeria wanavyohenyeshwa na Boko Haram, mfano wa Kbiti ni ushahidi tosha juu ya umahiri wa Jeshi letu.

JWTZ huna vigezo na hujahitimu uafisa kadeti nyota utaisikiaga tuu na kuiona kwa wengine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…