Hakika watu walisema kuwa wakizuiliwa kusema ya moyoni basi hata mawe yatasema.
Leo hii jijini Arusha kina mama wameamua kuyatoa yaliyo jaa mioyoni mwao juu ya Sabaya.
View attachment 1822827
Huyu bibi kama kweli ametoka nyumbani kwake mwenyewe na kutoa kilio hiki dhidi ya Ole Lengai Sabaya na matendo yake mabaya wakati alipokuwa DC pasipo kuandaliwa na watu ili watengeneze filamu feki, basi Sabaya hana pa kuponea na yatampata yote aliyoyatamka huyu bibi...
Amesema auae kwa upanga basi na yeye auwawe kwa upanga. Haya yalikuwa ya AGANO LA KALE wakati Wa sheria ya Musa. Kwa sasa Yesu Kristo anatuagiza "TUWAPENDE MAADUI ZETU, TUWAOMBEE"...
" Kuwapenda maadui zetu", Yesu Kristo alimaanisha tusipambane nao kwa nguvu za kibinadamu bali tuwaombee ili watambue makosa yao ili wapate neema ya kutubu dhambi zao...
Na pia Yesu Kristo anasema "mshahara wa dhambi (kuumiza wengine) ni mauti (kifo cha kiroho na baadaye cha kimwili)"
Aidha imeandikwa pia, "...kila dhambi atendayo mtu ina matokeo yake mabaya maana dhambi ilikwisha hukumiwa tayari". Madhara haya huwa juu ya aliyetenda dhambi hiyo. Ndiyo haya ya Sabaya...
Binafsi, namwombea Rehema na Neema Ole Lengai Sabaya ajue makosa yake, akiri kuwa alitenda ubaya na kisha ATUBU kwa Mungu wake, hakika atasamehewa...
Asije akawasikiliza wanaotetea matendo yake mabaya na kumtia moyo kuubeba ubaya. Mzigo ni wake, hana wa kumtetea kwa moyo na nia njema isipokuwa Yesu Kristo peke yake. Msikilize huyo vinginevyo atapata adhabu ya duniani na ile ya milele akiwasikiliza hao wanaojifanya kumpenda na kumtetea kwa upotovu....
Sisi sote ni binadamu. Tunapaswa kujifunza kwa mwenzetu na kubadilika na kuwa wanadamu wema dhidi ya wenzetu na uumbaji wa Mungu...