Video Clip: Rufiji litangazwe kuwa ni eneo la hatari na Serikali iwahamishe wananchi mara moja

Kuna watu hamnaga jema aisee...

Mafuriko mbona yapo kila mahali...
Tuache Tania hzi za kinaa...
 
Mimi ninachojua historia ya Maafuriko ya Mto Rufiji hayajaanza Leo,Ni kitu kimeanza tokea Mwaka 1968, Na Bwawa limepunguza kasi ya Maafiriko Kwa wananchi though Ni dogo, Kinachohitajika hapo Ni kuhamisha wananchi wote kutoka kwenye Hilo Eneo hatarishi wapewe Eneo Jingine Na Hilo Eneo la Bwawa la Mwalimu Nyerere litanuliwe Zaidi,Na ikiwezekana Eneo lote la Rufiji litengenezwe kuwa Benki ya Maji,Kwa sababu haiwezekani kushindana Na mkondo Wa Maji hata siku moja
 
Video yako ni ya kuwatisha wananchi sio
 
Mbona mko wepesi sana kwenye matusi jibuni hoja, hakuna bwawa ambalo halimwagi maji, hiyo iko kwenye kila bwawa duniani.
Hatukatai kumwaga maji kutoka kwenye bwawa, bali tunasema wananchi wahamishwe kutoka eneo hatarishi. Shirikisha kichwa chako kabla hujaanza kuandika
 
Sasa mkuu serikali haikutegemea result hizo za mapema, ndo maana hata wao wamedai walitegemea bwawa litajaa kwa miaka ila wonders ni kwamba limejaa kwa muda mfupi... Je, utawalaumu wao?
Hapo ndipo sasa kuhusisha wataalamu wa elimu ya mazingira kunapoonyesha umuhimu. Dikteta alisema mambo ya Environmental Impact Assessment yanachelewesha miradi!! Na nyinyi mkamshangilia
 
Watanzania tuna ujuaji wa kifara sana kwa kweli.
 
Mleta mada acha kuwachanganya watu kwa hiyo video. Hiyo video ninayo muda mrefu sana mimi na wala siyo ya leo wala jana.ila naona umeamua tu kuja kupigia propaganda hapa jukwaani kwa sababu zako binafsi.
Umekaa kukomalia picha badala ya ukweli wa taarifa. Lione kwanza!
 
W
Wewe acha kampeni za kuwaletea raia taharuki.

Hayo maji yanayoruka siyo yameachiliwa bali yamebanwa mahususi katika operesheni za kawaida kabisa za kuzalisha umeme.

Ili mitambo ifanye kazi ya kuzalisha umeme lazima ipate kani itokanayo na maji yanayopita kwa kasi.

Sasa wewe endelea kupotosha mburura wenzako na kuna kitu kipo nyuma ya pazia unakitafuta ama unakifanyia kazi.
 
Wapuuzi ni waliotunza maji bila ya kuyafungulia mapema yalipofikia kiwango chake cha mwisho. Ni aidha
a) Wamedhamiria Kuhujumu.
b) Wamefanya miscalculation.

Mvua za mwaka huu ni nyingi sana, wenyewe hata hawakutarajia kama maji yatajaa mwaka huu.
 
Your browser is not able to display this video.

Operation yakawaida kama hii
 
Mambo ya legacy hayo.Unachimba bwawa linazalisha mbu.Malaria inawagonga wananchi na vifo vinatamalaki.Ujinga plusplus!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…