Video: Huyu mstaafu aliwakosea nini Jeshi La Polisi? Kosa lake ni kukaa kijiweni?

Nyerere alitufanya kuwa watiifu mpaka tumekuwa wajing kiasi hiki, unakubali vipi kujibu maswali ya kijinga kama haya mbele za watu, ni kukataa tu kama wakupeleke polisi poa tu,
Wakenya hawakubali hata siku kuulizwa kama huu ujinga, wao ndio watamuuliza huyo polisi unanihiji kwa misingi, je nimefanya kosa lolote, kama hakuna, sikujibu, au nipeleke polisi itaeleweka zaidi huko
 
Wakuu,

Kuna video nimekutana nayo huko mtandaoni ya Afisa wa Polisi akiwa anamfokea mstaafu kwa kukaa kijiweni bila kuwa na kazi maalum.

Kwenye video hiyo, huyu Polisi kwanza kabisa anaongea na huyu mstaafu kama mwanae licha ya kwamba mstaafu umri wake umeenda na anasema kabisa aliacha kazi ya Upolisi kwa sababu ya hali ya kiafya.

Jeshi La Polisi ndo utaratibu wenu saivi ni kuuliza watu wanafanya nini vijiweni?

Soma pia: Rais Magufuli aagiza wastaafu Polisi kulipwa, asema wanaowacheleweshea haki ni wakubwa wao wanaokaa kwenye viyoyozi

Huyu mstaafu amewakosea nini mpaka mnamu-harass kiasi hiki?

Wapi imeandikwa kwenye katiba ni kosa kukaa kijiweni? Ibara ipi inamruhusu Polisi kumuuliza mstaafu kazi yake na kumuhoji kama mtuhumiwa?

Badala ya ku-deal na watekaji, wala rushwa na majizi serikalini mna-deal na wastaafu?

Kama hivi ndio mna-treat wastaafu basi we are working hard in a wrong country

POLISI NA ANDAZI CHAGUA ANDAZI UTANISHUKURU BAADAE
 
Lengo la kumhoji hadharani ni nini hasa?
1. Kumsaidia?
2. Kundhalilisha?
3. Hajui kuwa kuna watu wanatamani sana kufanya kazi lakini hawapati?
4. Kubeba mizigo si kazi?
5. Kuna Sheria iliyovunjwa na huyo mstaafu?

Sijui sana, lakini nahisi huyo Polisi kakosa uweledi! Anaongozwa na mihemko!
Form four failure,hawatumiagi akili
 
Wakuu,

Kuna video nimekutana nayo huko mtandaoni ya Afisa wa Polisi akiwa anamfokea mstaafu kwa kukaa kijiweni bila kuwa na kazi maalum.

Kwenye video hiyo, huyu Polisi kwanza kabisa anaongea na huyu mstaafu kama mwanae licha ya kwamba mstaafu umri wake umeenda na anasema kabisa aliacha kazi ya Upolisi kwa sababu ya hali ya kiafya.

Jeshi La Polisi ndo utaratibu wenu saivi ni kuuliza watu wanafanya nini vijiweni?

Soma pia: Rais Magufuli aagiza wastaafu Polisi kulipwa, asema wanaowacheleweshea haki ni wakubwa wao wanaokaa kwenye viyoyozi

Huyu mstaafu amewakosea nini mpaka mnamu-harass kiasi hiki?

Wapi imeandikwa kwenye katiba ni kosa kukaa kijiweni? Ibara ipi inamruhusu Polisi kumuuliza mstaafu kazi yake na kumuhoji kama mtuhumiwa?

Badala ya ku-deal na watekaji, wala rushwa na majizi serikalini mna-deal na wastaafu?

Kama hivi ndio mna-treat wastaafu basi we are working hard in a wrong country

Kukaa kijiweni ni haki ya kikatiba, hawa Polisi wanasumbua tu.

Hii habari inanikumbusha siku moja tulikuwa kijiweni Upanga.

Mara paap, tukaona polisi kama ishirini wanakuja na marungu yao na bunduki. Kwa mbali, mwanzo wa mtaa.

Nikawaambia madogo tuliokuwa nao, hapa wanabaki wazoefu tu, kama hamjiamini ondokeni. Wengine wakaondoka, wakubwa wa kijiwe tukabaki.

Basi wale polisi wakafika kijiweni. Wakatuuliza "Nyie mnafanya nini hapa?"

Mchizi wangu mmoja "Ngoto Spy" akawajibu "Nyie kwani ndivyo mlivyofundishwa kusalimia watu hivyo huko polisi?". Polisi walikuwa hawakutegemea jibu lile, wakastuka.

Wakaanza kutuuliza mmoja mmoja "Wewe unakaa wapi?" mtu anaonesha kwao, nakaa hapo, "wewe?" anaonesha, nakaa hapo.

Wakamfikia mwenye nchi mwenyewe sasa, maana kuna wananchi na wenye nchi. Wakamuuliza "wewe", akawaambia "Mimi nakaa kwa Baba Ben hapo". Polisi wakawa kama wanashangaa, "Kwa Baba Ben, kwa Baba Ben ndio wapi?". Akasema "Kwa Benjamin Mkapa wa Jamhuri ya Muungano, kwani kuna Ben gani mwingine?". Wakati huo Mkapa ndio kaanza urais.

Wale askari kwanza wakawa kama hawaamini. Ila, mmoja wao alikuwa anaenda kulinda kwa Mkapa akawa anamjua mchizi wangu, akawaambia ni kweli, huyu jamaa huwa namuona kwa Mkapa.

Basi wale polisi palepale kikawashuka. Unawaona kabisa ukali wote unawatoka, wanaanza kujipendekeza wanasema "Unajua wazee tulikuwa tunatambuana tu, ni katika kujuana tu". Haoo wakajikata.

Nasikia walipofika kituoni wana ramani kubwa ya eneo lile, wakaweka bonge la alama ya X kwenye kijiwe kile wakisema hiki kijiwe msikiguse, wanakaa watoto wa Mkapa hapo.

Nikasema polisi wa bongo ni waonevu sana, ingekuwa uswahilini pale hakuna mtu ambaye baba yake anajulikana wangewapa shida sana watu.
 
Wakuu,

Kuna video nimekutana nayo huko mtandaoni ya Afisa wa Polisi akiwa anamfokea mstaafu kwa kukaa kijiweni bila kuwa na kazi maalum.

Kwenye video hiyo, huyu Polisi kwanza kabisa anaongea na huyu mstaafu kama mwanae licha ya kwamba mstaafu umri wake umeenda na anasema kabisa aliacha kazi ya Upolisi kwa sababu ya hali ya kiafya.

Jeshi La Polisi ndo utaratibu wenu saivi ni kuuliza watu wanafanya nini vijiweni?

Soma pia: Rais Magufuli aagiza wastaafu Polisi kulipwa, asema wanaowacheleweshea haki ni wakubwa wao wanaokaa kwenye viyoyozi

Huyu mstaafu amewakosea nini mpaka mnamu-harass kiasi hiki?

Wapi imeandikwa kwenye katiba ni kosa kukaa kijiweni? Ibara ipi inamruhusu Polisi kumuuliza mstaafu kazi yake na kumuhoji kama mtuhumiwa?

Badala ya ku-deal na watekaji, wala rushwa na majizi serikalini mna-deal na wastaafu?

Kama hivi ndio mna-treat wastaafu basi we are working hard in a wrong country

Huyo officer anajiona mwamba sana anahisi atakuwa kijana milele
 
Kazi sana. Malipo hapa hapa duniani
 
Back
Top Bottom