Video: Huyu mstaafu aliwakosea nini Jeshi La Polisi? Kosa lake ni kukaa kijiweni?

Nyerere alitufanya kuwa watiifu mpaka tumekuwa wajing kiasi hiki, unakubali vipi kujibu maswali ya kijinga kama haya mbele za watu, ni kukataa tu kama wakupeleke polisi poa tu,
Wakenya hawakubali hata siku kuulizwa kama huu ujinga, wao ndio watamuuliza huyo polisi unanihiji kwa misingi, je nimefanya kosa lolote, kama hakuna, sikujibu, au nipeleke polisi itaeleweka zaidi huko
 
POLISI NA ANDAZI CHAGUA ANDAZI UTANISHUKURU BAADAE
 
Form four failure,hawatumiagi akili
 
Kukaa kijiweni ni haki ya kikatiba, hawa Polisi wanasumbua tu.

Hii habari inanikumbusha siku moja tulikuwa kijiweni Upanga.

Mara paap, tukaona polisi kama ishirini wanakuja na marungu yao na bunduki. Kwa mbali, mwanzo wa mtaa.

Nikawaambia madogo tuliokuwa nao, hapa wanabaki wazoefu tu, kama hamjiamini ondokeni. Wengine wakaondoka, wakubwa wa kijiwe tukabaki.

Basi wale polisi wakafika kijiweni. Wakatuuliza "Nyie mnafanya nini hapa?"

Mchizi wangu mmoja "Ngoto Spy" akawajibu "Nyie kwani ndivyo mlivyofundishwa kusalimia watu hivyo huko polisi?". Polisi walikuwa hawakutegemea jibu lile, wakastuka.

Wakaanza kutuuliza mmoja mmoja "Wewe unakaa wapi?" mtu anaonesha kwao, nakaa hapo, "wewe?" anaonesha, nakaa hapo.

Wakamfikia mwenye nchi mwenyewe sasa, maana kuna wananchi na wenye nchi. Wakamuuliza "wewe", akawaambia "Mimi nakaa kwa Baba Ben hapo". Polisi wakawa kama wanashangaa, "Kwa Baba Ben, kwa Baba Ben ndio wapi?". Akasema "Kwa Benjamin Mkapa wa Jamhuri ya Muungano, kwani kuna Ben gani mwingine?". Wakati huo Mkapa ndio kaanza urais.

Wale askari kwanza wakawa kama hawaamini. Ila, mmoja wao alikuwa anaenda kulinda kwa Mkapa akawa anamjua mchizi wangu, akawaambia ni kweli, huyu jamaa huwa namuona kwa Mkapa.

Basi wale polisi palepale kikawashuka. Unawaona kabisa ukali wote unawatoka, wanaanza kujipendekeza wanasema "Unajua wazee tulikuwa tunatambuana tu, ni katika kujuana tu". Haoo wakajikata.

Nasikia walipofika kituoni wana ramani kubwa ya eneo lile, wakaweka bonge la alama ya X kwenye kijiwe kile wakisema hiki kijiwe msikiguse, wanakaa watoto wa Mkapa hapo.

Nikasema polisi wa bongo ni waonevu sana, ingekuwa uswahilini pale hakuna mtu ambaye baba yake anajulikana wangewapa shida sana watu.
 
Huyo officer anajiona mwamba sana anahisi atakuwa kijana milele
 

Kazi sana. Malipo hapa hapa duniani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…