Duniatunapita man
Senior Member
- May 5, 2024
- 181
- 252
Dunia tunapita, na madaraka ni ya kupita
Ningependa anihoji mimi. Siku moja nilikuwa kwenye daladala kulikuwa na askari mmoja amevaa kombati, sasa akiongea jambo alikuwa akiwaambia walio karibu naye "sema ndiyo afande", basi nao walikuwa wakirudia anavyowaelekeza "ndiyo afande" na kujichekesha chekesa. Alivyoendelea hivyo, nilikuwa nasogea karibu naye ili na mimi aniambie "sema ndiyo afande". Baadaye gari lilisimama na akawa ameshuka. Sasa hata huyu ni hivyo. Si jukumu la polisi kumpangia mtu afanye kazi ya kufanya hata kama ina ujira mdogo, yeye jukumu lake ni kusimamia sheria, na kulinda raia na mali zao. Kama aliona hastahili kufanya hiyo kazi, si angmpeleka huko anakosema "mbona kazi ziko nyingi?" Anashangaa mtu kupata Sh10,000 kwa siku? Siku moja wakati narudi nyumbani kutoka kazini, nilichukua pikipiki. Ilikuwa kwenye saa mbili hivi usiku. Bodaboda akaniambia elfu 2 hadi nyumbani. Nilipofika nikampa hiyo Sh2,000, na akaniambia "sasa hivi ndiyo mara yangu ya kwanza kupata mteja na kulipwa elfu 2. Asante sana." Yaani siku nzima hadi saa 2 ndiyo hiyo elfu 2 niliyompa ndiyo alianza kupata. Sasa huyu bodaboda angehojiwa na huyo afande kusikia elfu 2, kama aliona elfu 10 ni ndogo si angezimia kabisa? Hata mimi nilishawahi kulipwa kiasi hicho kwa siku. Nilianza kazi Oktoba mwaka 2003 kampuni fulani kubwa kwa jina (siku hizi nadhani imeyeyuka). 'Take home' yangu ilikuwa Sh226,000 kwa mwezi, ila mshahara ulikuwa ukichelewa sana, yaana unalipwa baada ya miezi 3 kupita, na unalipwa mwezi wa mbele (mwezi mmoja tu) - kwa maneno mengine, ukilipwa, unabaki ukiidai kampuni miezi 3 (unalipwa mwezi wa nne mwanzoni au katikati) na kulipwa hela zote, labda uache kazi. Sasa ukichukua Sh226,000 kugawa kwa miezi 3 ni sawa na kulipwa Sh75,333.3 kwa mwezi na ni sawa pia na kulipwa Sh2,511.1 kwa siku. Sasa sijui angekutana na mimi akaniuliza unalipwa kiasi gani kwa siku, sijui angesemaje kama kwa huyo tu wa Sh10,000 aliona ni ndogo sana? Mimi niliyeajiliwa nilikuwa nalipwa Sh2,511.1 na huyu aliyejiajili Sh10,000 kwa siku. Halafu anasakamwa as if mtu unapenda ulipwe kiasi kidogo hivyo!