Video: Huyu mstaafu aliwakosea nini Jeshi La Polisi? Kosa lake ni kukaa kijiweni?

Dunia tunapita, na madaraka ni ya kupita
 
Polisi yuko sahihi,niaka 54 sio mzee aende akalime huko,watanzania wengi tuko wavivu,mzee wa ovyo kabisa huyo
Mtu kama hajafanya kosa ana haki ya kukaa popote ambapo ni public space Tanzania.

Hii ni haki ya kikatiba.

Suala la uvivu ni suala gumu kulijua, inawezekana huyo ni mwanafalsafa anafanya kazi ya kufikiri.

Na hata akiwa mvivu, mtu ana uhuru na haki ya kuwa mvivu, ilimradi hajaiba cha mtu, akiwa mvivu mwacheni tu atapigika ajifunze mwenyewe.

Kwani mtu akiwa mvivu katika maisha yake mwenyewe hajakuibia kitu tatizo lako nini?

Zaidi, mtu ana haki ya kukataa kusema kazi yake ni nini. Kuna watu kazi zao ni biashara za siri wakizisema watavujisha "trade secrets" zao, mtawaiga na kuwaharibia uwezo wao wa kutengeneza pesa, sasa hao kwa nini mnawalazimisha wawaambieni kazi zao bila hata warrant ya kimahakama?
 
yule JWTZ
Kwani jeshi unastaafu kwa miaka mingapi? Miaka 54 kwa waajiliwa wa umma unatakiwa uwe kazini!
,kasema alistaafu kwa UGONjwa sio kwamujibu ,hivyo muroto alitakiwa kuelewa hivyo ,kamkosea sana JWTZ wetu mimi kwa kuangalia video tu nimegundua mwamba mgonjwa muroto alitakiwa awambie wasaidizi huyu mwamba mkaenae kule harafu mzungumze nje ya kamera.
 

Mkuu usipoteze muda wako.

Kuna watu ni senile and competent kwenye kufikiri watakupotezea muda
 
Hahahahaaha ni yeye mkuu huyu mzee alikuwa ananivunja mbavu sana alivyokuwa anawahoji wahalifu mbele ya kamera, kwa hapo mzee muroto ni mtu mzima zaidi ya huyo askari na nadhani walimpanga tu kuamsha amsha maana alikuwa anapenda sana.
Hiyo sauti ni kama ya aliyekua kamanda wa mkoa wa Dodoma Gilles Muroto,ambaye hata yeye sasa hivi ni mstaafu,

Nakumbuka ile kauli yake ya "Kipigo watakachokipata ni cha Mbwa koko''
 
Huyu polisi ni mpumbavu!
Hiyo siyo kazi yake !

Polisi kumejaa wajinga,failure.
 
Ni kweli kabisa! Kazi ya polisi si kuuliza watu wanafanya kazi. Hata angeulizwa na mtu mwingine (kama amevaa kiraia) huenda hawezi kusema yeye ni polisi. Yeye anaona kulipwa Sh10,000 ni ndogo sana kwa mtu wa miaka 54. Kitu ambacho angefanya ni kumsaidia kutafuta kazi yenye kipato kizuri zaidi. Kwenye posti moja hapo juu nimesema niliajiliwa kwenye kampuni moja kubwa hapa Tz na 'take home' yangu ilikuwa Sh226,000, lakini tulikuwa tunalipwa baada ya miezi mitatatu (yaani mwanzoni mwa mwezi wa nne au katikati). Ukichukuwa Sh226,000 na kuigawa kwa miezi 3, utapata kwenye Sh75,000+ kwa mwezi na kuigawa kwa siku ni sawa na Sh2,51.1 kwa siku. Sasa kwa huyo mstaafu aliona Sh10,000 kwa siku ni ndogo, sijui kwangu wa Sh2,51.1 kwa siku angesemaje?
 
Mkuu usipoteze muda wako.

Kuna watu ni senile and competent kwenye kufikiri watakupotezea muda
Sipotezi muda.

Nafundisha haki za kikatiba kuna watu wanasoma na kujifunza.

Na wakijifunza mimi sioni hilo kuwa ni kupoteza muda.

Watanzania wengi wana uelewa mdogo sana kwenye haki za kikatiba na kibinadamu.

Huyo polisi anayemnyanyasa polisi mwenzake mstaafu hajui kuwa miaka michache ijayo na yeye anaweza kujiunga naye hapo kijiweni.
 
Yani hata kama kijana, achikia mbaki mstaafu, angekuwa kakaa kijiweni anacheza bao tu hapati hata shilingi 0, bado ingekuwa haki yake.

Polisi anatakiwa kufuatilia wahalifu, sio watu waliojikalia vijiweni kwa kukosa au kutotaka kazi.

Ni hivi, mtu kukataa kufanya kazi ni haki yake ya kibinadamu. As long as hajafanya uhalifu tatizo liko wapi?
 
Polisi mstaafu hawezi kukosa kazi ya kufanya kwani wanajuwa njia nyingi za utapeli na ujambazi pia. Ndiyo maana baba yangu aliniambia never trust a police man, si watu wazuri hata akistaafu.
 
 

Attachments

  • IMG-20241125-WA0017.jpg
    131.8 KB · Views: 1
KAZI ya kuchimba mashimo ya choo mjini ina fedha kuliko KAZI ya poli.....
 
🤣 mwana unawachukia manjagu. sema usikute naye enzi zake alikua mkuda. isijekuta tunapoteza muda kumuonea huruma.
Alikuwa mkuda huyo hiyo ni laana ya aliodhulumu haki zao
Polisi wengi huwa na mwisho wa mauzauza
 
What is this Jeshi la polisi jamani embu mliangalie hili hii inachafua image yenu.Kweli unaongea na mstaafu namna hii kama mtu aliyelewa maadili ya kwapi?Na kaita na vyombo vya habari kabisa bila kuona haya.Binafsi sijamaliza kuangalia hii video hii inasikitisha kwa kweli.Jeshi la polisi mjitafakari kuhusu hili huu ni ukosefu wa utu na maadili!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…