Ustadhi kwamba hapo umekaa unafikiri hilo halifahamiki Ukraine, kwa taarifa yako utakuta hao ni navy SEALS, SAS na makomando wengine wa kutokea mataifa ya magharibi ambao hawawezi kuhusishwa rasmi, inabidi waingizwe kwa namna ya kujitolea, sasa huyo unayesema kachero Mrusi ajipenyeze ndani ya hao.
Nashuku hata ndio maana jeshi la Putin limeshindwa kuteka mji wa Kiev, wanakutana na mapigo ya kikomando ambayo hawakua wamejiandaa....Halafu sasa hawa hapa chini ndio wanajeshi wa Urusi waliotolewa kafara na Putin kutangulia frontline, vitoto vidogo vimekamatwa vingi sana hadi huruma....Inabidi mama wao huko Urusi wapige simu kuwaliwaza maana wataanza kulialia.