Video: Makonda yamkuta makubwa, Ghalib wa GSM adai nyumba yake

Video: Makonda yamkuta makubwa, Ghalib wa GSM adai nyumba yake

Huihui2

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2012
Posts
7,021
Reaction score
11,475
Mwaka 2019 aliwadanganya GSM wale wafadhili wa Yanga kuwa Jiwe anataka ajengewe nyumba. Kweli GSM wakamuamini na wakajenga.

Baada ya hapo GSM wakawa wanataka Jiwe mwenyewe akazindue nyumba hiyo lakini Bashite akawa anawapotezea. Ndipo kwa namna yao wakamfikia Jiwe na mchezo ndipo ulipoharibika kwa vile Jiwe hakumtuma Bashite.


 
Hao GSM nao wana record mbovu tu, hapo naona tapeli nae katapeliwa.

Kila nikisoma ule uzi wao ulioko huku JF naona hao jamaa nao wanatakiwa kuchunguzwa na vyombo vya dola, ni wahalifu wanaolindwa na urafiki kati yao na walioshika hatamu.

GSM na Makonda wote marafiki wa Ikulu, shikeni majembe yenu mkalime tu.
 
Mnapenda uchonganifu na umbea. Fanyeni kazi muda wa kazi huu
Unadhan wote tunafanya Kaz zinazofana mkuu. Mm natoka lindo mda huu nimekesha usiku kucha

Halafu acha kukalili wengine mda huu ndio saa moja usiku baadh ya nchi japo mm nipo hapahapa kwa nyerere

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
mtanzania mweusi anapambana na Makonda dhidi ya tajiri Msomali Gharib....

Huyu Gharib na GSM sidhani kama wana nguvu yeyote ya kumnyoshea kidole Makonda
Sio kidole tu bali wameshachukua nyumba yao aliyotaka kuwatapeli kwa mgongo wa JPM na ni wazi bashite hana cha kuwafanya.

GSM ni vijana wa msoga hawakosi back up ya riz ambaye ni naibu waziri wa ardhi na makazi.
 
Makonda leo nae analalamika??? Kweli Dunia duara....Jengo lenyewe linaonekana halijaisha...Lakini Kupitia Makonda watu wajifunze ubaya hapa Duniani haudumu na ukitenda ubaya utaulipia kabla hujafa...kingine cheo hakidumu heshimu watu...
Makonda alikua anaogopwa ila hakuheshimika leo analalama analia na kudhalilika...Upande wa pili akiulizwa Mali kama hiyo wewe Mtumishi wa Umma umekua tu DC na RC umepata wapi?? Hatakua na majibu..

Watumishi wa Umma mjifunze hao watu huwanyenyekea na kujifanya marafiki lakini urafiki wao ni wa cheo chako sio wewe hivyo kuweni makini hao watu sio.
 
Back
Top Bottom