Video: Makonda yamkuta makubwa, Ghalib wa GSM adai nyumba yake

Video: Makonda yamkuta makubwa, Ghalib wa GSM adai nyumba yake

Hao GSM nao wana record mbovu tu, hapo naona tapeli nae katapeliwa.

Kila nikisoma ule uzi wao ulioko huku JF naona hao jamaa nao wanatakiwa kuchunguzwa na vyombo vya dola, ni wahalifu wanaolindwa na urafiki kati yao na walioshika hatamu.
GSM ndo KIKWE..... NDO HELA ZA SHOPPING CENTER ZILIPOFICHWA NDO HAO WALIO IUA KARIAKOO KWA KUONDOKA NA MITAJI YA WAFANYA BIASHARA NDO WAKWEPA KODI WAKUBWA
 
Makonda alikuwa tapeli wa kiwango cha juu. Kule Mwanza alipora kiwanja Capripoint kutoka familia ya Chacha, mmiliki wa hospitali ya CF. Akawadanganya kuwa watalipwa, akaishia kujenga nyumba yake binafsi.

Hao nao watakuwa wajinga Kama hawatamshtaki.
 
Makonda alikuwa tapeli wa kiwango cha juu. Kule Mwanza alipora kiwanja Capripoint kutoka familia ya Chacha, mmiliki wa hospitali ya CF. Akawadanganya kuwa watalipwa, akaishia kujenga nyumba yake binafsi.
Si alifariki huyu dokta Chacha? Aisee Makonda basi atakuwa ana visasi kwa watu wengi sana na itamu hunt sana
 
Ukienda TAKUKURU Upanga kuna watanzania wenye asili ya India kama watano walileta malalamiko pamoja na kadi za gari... Kuna mmoja alichukuliwa new model v8 ya mwaka 2016 na bei yake mpaka leo ipo juu sana hiyo gari..

Hawa walikuwa wanalindwa na mfumo ulivyokuwa wa nchi...

Kwani watu hawakusikia msemo huu ' KWENYE UONGOZI WANGU TAJIRI ANAFANYWA CHOCHOTE ' na watu wakapiga makofi..

Bora hawa wakina GSM wamesalimika na roho zao.... Matajiri wengi walifariki wa pressure kitokana na kuambiwa inahitajika hii.. Account yako inatakiwa ikatwe hela hii.....

Hujakaa sawa unafuatwa mheshimiwa amenituma kwako kuchukua hiki... Nk

Nadhani Mungu alikuwa na makusudi kufanya alichofanya. Maana vilio vya ndani vilikuwa vingi Sana.
 
Nadhani GSM kama wana akili waache kucheza michezo ya wanasiasa. Hakuna aliyejua Nape atakuja kuwa Waziri karibuni.

Makonda anaweza kuja kuwa Rais au Waziri na mwenye ma mlaka ndipo utakapoona GSM wanakimbia nchi.

Huyo huyo nape aliondolewa uwaziri kisa makonda. Mimi nassuport GSM wakadai nyumba yao maana kudai Mali yako hakuna uhusiano na kuwa uRais na uWaziri was mtu.
 
Huyo huyo nape aliondolewa uwaziri kisa makonda. Mimi nassuport GSM wakadai nyumba yao maana kudai Mali yako hakuna uhusiano na kuwa uRais na uWaziri was mtu.
Mkuu wanasiasa si watu wa kuweka nao bifu hasa unapokuwa mfanya biashara. Kama GSM wana mtu wa PR wataliona hili nalosema. Hivi nani alijua Makala atakuja kuwa mkuu wa mkoa wa Dar???? Ninachomaanisha hapa ni kuwa wanasiasa wana mitaji mikubwa ya network, mtu anaweza kuwa idle kwa muda ila siku mtu wake akimkumbuka basi anaweza kulipiza kisasi. Msipe kichwa GSM. Na kumbukeni Makonda na Mama ni kitu kimoja.
 
Nadhani GSM kama wana akili waache kucheza michezo ya wanasiasa. Hakuna aliyejua Nape atakuja kuwa Waziri karibuni.

Makonda anaweza kuja kuwa Rais au Waziri na mwenye ma mlaka ndipo utakapoona GSM wanakimbia nchi.
msomeni huyu mpuuzi hapa 🤣🤣🤣
kwa hiyo ukidhulumiwa na mwanasiasa utulie tu. akitaka hivyo akamdhulumu mama yake wamalizane kindugu
 
Back
Top Bottom