sengobad
JF-Expert Member
- Aug 13, 2017
- 9,008
- 8,788
Hebu jitose kama KubeneaKama serikali iliamua kumfungulia kesi za kutosha Sabaya sioni ni kwanini Makonda ambaye ni zaidi ya Sabaya serikali hiyo hiyo inapata kigugumizi cha kumfungulia kesi. Mbona ni swala rahisi sana ni kiasi tu cha kutangaza kuwa kila mwenye ushahidi awasilishe polisi au takukuru basi biashara imeisha. Ikitokea ushahidi haujitoshelezi basi aachiwe na mahakama imsafishe aachwe aendelee na maisha yake kama kawaida.
Lakini hii habari ya kuacha kila mtu aende binafsi kumdai Makonda naona kama linaichafua serikali na ni hatari kwa maisha ya Makona kwani sio wote watakaenda kudai mali zao kistaaarabu hasa ikitokea kama kweli kuna mtu ana madai halali halafu alidhulumiwa kibabe kwani kila mtu anajua yaliyokuwa yanatokea kipindi hicho.