VIDEO: Mbowe, Lissu wasalimiana kibabe BAWACHA, huku wakicheza kwa bashasha wimbo wa "Tuvushe Mbowe Tuvusheee"

Leo kwenye mkutano wa BAWACHA Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu wameonekana wanasalimia kwa bashasha. Wakati jana tu Lissu katoka kumshushia maneno makali sana na tuhuma kibao mwenyeketi wake halafu leo ety kwa madai yao wanaonyesha wapo sawa.

Mh ndiyo maana nimesema hichi chama tena akipewa huyu Lissu ndiyo kwaheri kabisa CHADEMA katika ramani ya siasa nchini. Maana ajuhi kujishikilia kwenye siasa za kistaarabu anahisi kuropoka kwake ndiyo silaha kumbe ni ujinga mtupu!

CCM ni namba moja. Mama Samia mitano tena! Mpaka 2030

Snapinst.app_473756179_980056560685872_1017043660594601711_n_1080.jpg
 
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu wakisalimiana katika mkutano mkuu wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha) unaofanyika leo Alhamisi Januari 16, 2025 katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.

Wote wawili wanamchuano mkali kuelekea Uchaguzi wa nafasi ya Uenyekiti CHADEMA unaotarajiwa kufanyika Januari 21.
Pia, Soma:
-
PICHA: Mbowe, Lissu walivyokutana uso kwa uso kwenye Kikao cha Kamati Kuu Chadema
- Uzi maalumu wa matokeo Uchaguzi wa Baraza la Vijana (BAVICHA) na Baraza la Wazee (BAZECHA) na wanawake (BAWACHA) CHADEMA Taifa 2025
Kama hapo walipo hawana kinyongo basi nashauri tarehe 21 wasalimiane tena hivyo hivyo na Wenje pamoja na mzee wa mizimu Yeriko wawepo hapo katikati bila kusahau wale Covid 19
 
Kinachonishangaza na kunichekesha ni kwamba 95% ya nyumbu wanaitaja ccm kwenye hoja yao hii ambayo ccm Wala haipo na Wala haihusiki na Wala haijui kama Kuna watu huko wanahangaika na wanachokiita 'uchaguzi'.

Enyi nyumbu, hakuna muda ambao ccm ingepata mtikisiko kama 2015 wakati wa Lowassa. Je, kilitokea nini'?!!! Nitawasaidia kujibu, kikundi chenu Cha kikoba kiliathirika......slaa alitoka na mpaka Leo hajakaa sawa.

Mnajua nini nyie nyumbu?!!! Hakuna muda ambao ccm itapata urahisi wa kushinda kama mwaka huu 2025, hususani ikitokea huyo mwenye jina lenye maana sawa na 'tobo' akichukua kiti. Mnajua itakuaje?!!' Ni rahisi tu, wanampa uongozi wa timu ya kampeni Makonda basi. Kazi inakuwa imekwisha na watu wanatulia tuliiii wanajipigia miluzi tu. Huyo Makonda peke yake anamtosha.
 
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu wakisalimiana katika mkutano mkuu wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha) unaofanyika leo Alhamisi Januari 16, 2025 katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.

Wote wawili wanamchuano mkali kuelekea Uchaguzi wa nafasi ya Uenyekiti CHADEMA unaotarajiwa kufanyika Januari 21.
Mbowe na Lissu wakifurahia katika mkutano mkuu wa wanawake CHADEMA
Pia, Soma:
-
PICHA: Mbowe, Lissu walivyokutana uso kwa uso kwenye Kikao cha Kamati Kuu Chadema
- Uzi maalumu wa matokeo Uchaguzi wa Baraza la Vijana (BAVICHA) na Baraza la Wazee (BAZECHA) na wanawake (BAWACHA) CHADEMA Taifa 2025
Hivi mmegundua Mh Mbowe amevaa Lile gwanda la mwaka 2005 wakati akigombea Urais kwa Kampeni za Chopa?
😅
 
Lilissu linafurahisha Sana embu lione linavyoyarudi bila wasiwasi likitoka hapo linaenda kumchamba bwana Mbowe Ila hapo lipo linacheza wimbo wa mwamba tuvushe .

Inahitaji uvumilivu wa akili na kichwa .
 
Mnajua nini nyie nyumbu?!!! Hakuna muda ambao ccm itapata urahisi wa kushinda kama mwaka huu 2025, hususani ikitokea huyo mwenye jina lenye maana sawa na 'tobo' akichukua kiti. Mnajua itakuaje?!!' Ni rahisi tu, wanampa uongozi wa timu ya kampeni Makonda basi. Kazi inakuwa imekwisha na watu wanatulia tuliiii wanajipigia miluzi tu. Huyo Makonda peke yake anamtosha.
Lisu mwenyewe akihojiwa kasema uraisi kwake sio rahisi kushinda sababu ya blabla za tume huru ila Chadema ndiko kajipanga kushinda

Huu uchaguzi wa Chadema Lisu kau personalize kuwa ni vita kati yake na Mbowe badala ya chama

Mbowe upande wake na tomu yake wao wanatafuta viongozi wa Chama sio personal kuwa kampania Lisu

Kistratejia Mbowe yuko vizuri sababu muono wake ni wa kichama zaidi sio.sijui vita yake na Lisu Hana hilo
 
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu wakisalimiana katika mkutano mkuu wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha) unaofanyika leo Alhamisi Januari 16, 2025 katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.

Wote wawili wanamchuano mkali kuelekea Uchaguzi wa nafasi ya Uenyekiti CHADEMA unaotarajiwa kufanyika Januari 21.
Mbowe na Lissu wakicheza kwa furaha katika mkutano mkuu wa wanawake CHADEMA (BAWACHA)
Pia, Soma:
-
PICHA: Mbowe, Lissu walivyokutana uso kwa uso kwenye Kikao cha Kamati Kuu Chadema
- Uzi maalumu wa matokeo Uchaguzi wa Baraza la Vijana (BAVICHA) na Baraza la Wazee (BAZECHA) na wanawake (BAWACHA) CHADEMA Taifa 2025
Kumbe hamtaki wasalimiane wakisalimiana inakuwa habari!
 
Hakika Mbowe ninkama maji, usipoyanywa utayaoga.

Bawacha leo wameweka wimbo wa "tuvushe Mbowe tuvushe". Baada ya wimbo huo kupigwa Lissu alisimama haraka kwenye kiti na kuanza kusakata dansi huku akikata mauno.

Hakika Mbowe ni tunu ya taifa.
 
Hahaha ila hawa watu jamaniiii mbona siwaelewi
 
Back
Top Bottom