VIDEO: Mlinzi wa Rais Samia alivyotaka kudondoka wakati Rais akihutubia

VIDEO: Mlinzi wa Rais Samia alivyotaka kudondoka wakati Rais akihutubia

Hapo kwenye kujikaza ndipo alipokosea.Watu wengi tunashindwa kupata msaada mapema kwasababu ya kujikaza.Mtu unajisikia kabisa hauko sawa lakini unaogopa kusema unaishia kuanguka mbele za watu.Uoga na uvumilivu kwenye afya zetu zinatuumiza wengi.
 
Hakuna mtu aliyepitia mafunzo anaweza kuanguka kizembe hivyo ? Maana wanafanya kazi kwa shift sio kuwa kila siku ni yeye. Na cha kuongezea wanaenda mafunzo magumu sana ndiyo maana nikasema ni nepotism. Hili swala halipo tu kwenye ulinzi mpaka katika sekta nyingi za serikali. Vitu vinafanyika mkuu wa Idara anapitisha na hajui amesign nini ? Yaani mpaka unajiuliza huyu amepata hiki cheo ?
Mafunzo magumu na kuumwa au kupata dharura yakiafya wala haviusiani.Ndo maana ata uko kwenye mafunzo madaktari wa dharura wanakuwepo kwasababu mwili unaweza kupata changamoto yoyote kwa yoyote wakati wowote.Hiyo nepotism baki nayo kwasababu ni mtazamo wako ila jua binadamu sio robot.
 
Ndugu hakuna kutetea ujinga vitu vinatakiwa vifanywe kwa mpangilio. Kama kuumwa inabidi kitengo kijue na hawa walinzi wapimwe kila wiki. Kuna nchi walinzi wa rais wanaopangiwa hadi aina ya chakula wanachokula. Narudia tena kuna Makonda wa daladala na walimu wanasimama siku zima inakuaje mlinzi aliyepita mafunzo ashindwe kusimama kwa masaa machache ?
 
Huu usawa tunaulazimisha ila kiukweli ni kazi ngumu Kwa mwanamke kusimama muda mrefu
Iwepo division of labor, majukumu ya ulinzi yafanywd na wanaume
Mwanaume kuwa bodyguard wa rais mwanamke nadhani haina Afya. Labda muda wa zamu ya kumlinda uangaliwe!
 
Makonda wa daladala , Walimu wanasimama siku nzima na bila mafunzo ya kijeshi. Kuna watu mtaani wakipewa nafasi ya kupitia mafunzo watafaulu kwa viwango vya juu. Haya ndiyo matokeo ya kupeana kazi kwa kujuana, bodyguard wa rais anaanguka. Hajapigwa risasi wala kunywesha sumu, Je Rais yupo salama ?
Mwalimu gani husimama siku nzima?..konda saa sita mpaka aaa nane huachia deiwaka,saa nne mapumziko chai
 
Hii ni kawaida, huyo dada ni shujaa na mfano wa kuigwa. Amepambana kusimamia jukumu lake hadi sekunde ya mwisho. Ile movement wakati anaishiwa nguvu ingekuwa wewe raia ungeshadondoka kama gunia.
 
Kama huyo bodigadi ameshindwa kazi aseme kuna walimu na makonda wanasimama siku nzima yeye ameshindwa kusimama kwa masaa machache na ni mwanajeshi are we serious ? Kuna watu wanatafuta kazi na ukiwapa nafasi ya kufanya mafunzo ya kijeshi wanapita kwa viwango vya juu. Tatizo hizo nafasi wanapeana wao kwa wao .
Nyumbani kwenu hakuna wanawake?, huna madada au wadogo zako wa kike?.

Hao ni wapambe tu walinzi halisi wa Samia huwa wanajaa kila mahali anapokuwepo.

Sio suala la nafasi kupeana kindugu kuna suala zima la ubinadamu wa huyo anayepewa nafasi. Wanakufa watu wakiwa ndani ya gym mazoezi yakiendelea sembuse huyo mama aliyepata kizunguzungu!.
 
Hii ni kawaida, huyo dada ni shujaa na mfano wa kuigwa. Amepambana kusimamia jukumu lake hadi sekunde ya mwisho. Ile movement wakati anaishiwa nguvu ingekuwa wewe raia ungeshadondoka kama gunia.
Sukari inaposhuka au kupanda inaleta kizunguzungu. Tunatembea na matatizo kibao mwilini.
 
05 Aprili 2025
Judiciary Square
Dodoma, Tanzania

Tazama mlinzi wa Rais Samia alivyotaka kudondoka wakati Rais akihutubia

Tukio hili limetokea leo Aprili 5, 2025, Dodoma, wakati Rais Samia Suluhu Hassan akizundua majengo ya mahakama ya Tanzania.

View attachment 3294214
Inawezekana ikawa ni uchovu kutokana na aina ya kazi ulinzi wa viongozi, hivyo kukosa nafasi ya mapumziko au kutopata vimiminika kama maji n.k vya kutosha mwili usizimike.

TOKA MAKTABA :
21 Oktoba 2019

Baadhi ya matukio karibu na rais yaliyozua mjadala mpana wa umma :

Ruangwa Lindi Tanzania ziara ya John Magufuli, walinzi wafanya maamuzi baada ya moshi kujitokeza unaoweza kuleta hali yoyote isiyotegemewa

Rais azingirwa na moshi unaoonekana kwa macho, pia kuna uwezekano wa hewa kuzingirwa na vitu au hewa isiyoonekana kwa macho

MOSHI / HEWA YAVURUGA MKUTANO WA RAIS MAGUFULI RUANGWA,MLETE HUYO ALIYEWASHA​

View: https://m.youtube.com/watch?v=IiWbvuPFcps

Pamoja ya kuwa wananchi waliokuwepo eneo kutahayari kuona tukio la moshi la 'ajabu' ukimzingira rais, iligundulika moshi huo ni wa fire extinguisher/ kifaa cha kupuliza kuzima moto, lakini mkutano huo wa njiani wa kusimamishwa ukaghahirishwa bila kusita kwa mujibu wa protocol zilizomo ktk mabuku ya vyombo vya 'vitengo' ili kubaini ni kifaa cha zimamoto au la n.k

Hii ni pressure,akipata drip za maji or oxygen ya kutosha atarejea plus kulala/pumzika angalia mwili wa aliekuja simama badala yake ulivyomdogo.
 
Unataka kuniambia muda ambaao Makonda na walimu wanasimama unazidi muda ambao Rais anahutubia ?
Unadhani huyo kaanza kusimama hapo tu? Mazoezi yao hao hawalali siku tatu,kusimama juani toka saa sita mpaka kumi jua la dodoma tena sometimes uchi wakitazamana jinsia tofauti,hapo ni ubinaadam tu umetokea
 
Nyumbani kwenu hakuna wanawake?, huna madada au wadogo zako wa kike?.

Hao ni wapambe tu walinzi halisi wa Samia huwa wanajaa kila mahali anapokuwepo.

Sio suala la nafasi kupeana kindugu kuna suala zima la ubinadamu wa huyo anayepewa nafasi. Wanakufa watu wakiwa ndani ya gym mazoezi yakiendelea sembuse huyo mama aliyepata kizunguzungu!.
Hao wanaokufa Gym wanatumia steroids mimi naongelea mfanyakazi alieajiriwa na taasisi kumlinda kiongozi wa nchi.
 
Kwa hio unataka kuniambia Rais yupo kwenye GARI yeye alikuwa siti ya mbele kasimama ? Kuna watu kib ao mtaani hawana ajira haya mambo madogo sana kwao. Tembea uone
Hao kulala ni mpaka rais alale na pengine hawalali,wanaamka kabla yake,anajiandaa ndani 3 hrs before wao wapo wima,wameandaliwa kwa kazi hiyo, mazoezi aliyopitia huyo mwanamke wewe huyawezi
 
Ubinafsi unakusumbua
Unataka mwanamke awe mwanajeshi lakini sio mama yako, mke wako, Binti yako, shangazi yako
Mwanamke hapaswi kufanya kazi ngumu
Ni vizuri kwamba unajua kwamba mimi ni mbinafsi. Kati ya mimi na wewe nani ni mbinfsi?. Mimi nasema swala la kuwa mwanajajeshi halina uhusiano na jinsi ya mtu na wewe unasema mwanamke hapaswi kuwa mwanajeshi.

Hili la mama, mke, binti au shangazi umelijuaje? Una hakika gani na unayoyasema? Mimi nikisema una superiority complex ninaoushahidi wa haya maandiko yako kwamba mwanamke hapaswi kuwa mwanajeshi wakati wako wanawake ambao ni wanajesghi wenye vyeo vikubwa. Haya yako wewe huoni kwamba ni kichekesho?
 
Hao kulala ni mpaka rais alale na pengine hawalali,wanaamka kabla yake,anajiandaa ndani 3 hrs before wao wapo wima,wameandaliwa kwa kazi hiyo, mazoezi aliyopitia huyo mwanamke wewe huyawezi
Kazi zipo kwa shifti ndugu naomba unitajie Bodyguard wa wa waziri mkuu wa Israel au wa nchi inayojielewa ameanguka nasubiri hapa ndugu ?

Mtu aliyepita kozi kisawasawa special kwa ajili ya kumlinda Raisi hawezi kuanguka wala kuzima. Huyu amebebwa na amepewa kazi kwa kujuana na haya mambo yapo mengi sana jeshini, usalama wa taifa na polisi. Kwa hiyo mimi sishangai yeye kuanguka hana vigezo kubebwa full stop.
 
We jamaa kiazi sana,kwa hiyo israel ndiyo kipimo chako?..hapa inaonesha nazozana na bogus kiasi gani
 
We jamaa kiazi sana,kwa hiyo israel ndiyo kipimo chako?..hapa inaonesha nazozana na bogus kiasi gani
Wewe leta facts ndugu huyo kabebwa angekuwa mwanajeshi wa kawaida kwenye gwaride sawa. Mtu anakula mlo mmoja naRais analala hoteli moja na rais. Halafu anazima ghafla kisa uchovu , are we serious ? Mtu aliyepitia mafunzo makali anapata kitengo cha kutembea na rais halafu anazima ? Je angekuwa askari wa kukimbia rutemach kila siku asubuhi ? Angekuwa askari wa kupewaa mazoezi ya kushtukiza kila siku ? Aisee Usalama wapunguze nepotism kuna vijana kibao wako mtaani hio kazi wanaiweza aisee. Kama vipi wasiende mtaani waende hata hapo Ngerengere92 KJ. Au kama wakishindwa waende wakachukue wa Kagame kama JPM. Ikiwezekana afukuzwe kazi mapema asubuhi.
 
Back
Top Bottom