Uchaguzi 2020 Video: Polisi wakisindikiza msafara wa Lissu unaoshangiliwa na kupungiwa mikono na maelfu ya wananchi

we nani mpaka uwapangie watu cha kuandika
 
Mungu kasimama upande wa LISSU hata wakusanye wapiga manyanga Mungu yuko kwa LISSU TU

Mungu hayuko kwa Lissu tu, acha hizo, Mungu yupo kwa kila mmoja wetu, hata kwako na kwangu, kwa huyu na yule, Mungu yupo.. Ila najua concern yako, mahaba makuu juu ya Lissu yamekufanya uandike hivyo na kukosea.
 
Umemjibu vizuri sana huyu nyumbu.yani mtu asome vitabu vyote hivyo na majukumu yake yakazi yawe palepale kana sio uongo huo[emoji23]
 
Eti pesa inakata! Hivi unadhani sasa hivi ni kama zamani? Kijana asiye ajira miaka mitano toka atoke chuo, mstaafu anayesotea mafao, mkulima asiye furaha au mfanyabiashara aliyefunga biashara kwa kunyanyashwa na TRA pia mtumishi asiyepanda daraja au mshahara hao wote wanasubiri kumuona Diamond au TOT jukwaani ndio kutoa kura?

Hao wote Magufuli hata aruke samasoti jukwaani au acheze kiwanzensa hawawezi kumchagua. Sio kwa sababu Lissu ni kiongozi mzuri sana la hasha, bali kwa sababu Magufuli ni kiongozi mbovu sana kwa nafasi ya urais
 
Ndio hawa waliokuwa wanasema upinzani/CHADEMA imekufa!!!
Vijijini ambako Kuna asilimia 80 ya wananchi kuna Chadema?

Chadema Ina vitawi vichache tu mijini kwenye baadhi tu ya miji Tanzania ndio maana hata wadhamini anaenda kwenye baadhi ya miji
 
Ukimiliki gari na nyumba wewe ni tajiri na una amani wewe ni tajiri.
 
Serikali haina haja ya kuwatafutia wapinzani sababu ya kuongea..
 

Hiyo ni Mikumi, Morogoro siku ya jana akiwa njiani kuelekea Iringa.
Mungu alipanga mwisho wa CCM kwa namna ambayo akili ya mwanadamu haiwezi kuelewa kirahisi. Aliamua aje mtu mgeni kwenye chama (Magufuli) ambaye atawanyang'anya chama wakongwe (Makamba, Kinana, Kikwete, Membe nk) na kuingiza watu wake wapya (Bashiru, Makonda, Polepole).

Hawa wapya kwa namna yake watakivuruga chama na misingi yake kwa maagizo yake Mafufuli. Wataleta chuki na maovu kama utekaji (Mo Dewji, Roma ) na uuaaji (Ben Sanane, Azory Gwanda nk).

Halafu watamshambulia mmoja wa viongozi wa upinzani (Lissu) kwa risasi za bunduki ya vita lakini mtu huyo hatokufa. Nchi nzima itashangaa namna mtu huyo alivyoshambuliwa, kunyimwa matibabu, kunyang'anywa mshahara kisha kufukuzwa ubunge.

Wanaposhangaa hayo na kumhurumia ndiyo watataka awe Rais wao wa 2020-25. Mungu ana sababu kwa kila jambo. Mwisho wa CCM ni mwaka huu. Alilopanga Mungu Binadamu hawezi kubadilisha. Hata kama NEC itaiba kura na kumtangaza Maguduli, nguvu ya umma itamtoa tu Ikulu. Wananchi wamechoka maonezi, dhuluma, ukandamizaji, ubaguzi na dharau
 
Huu ni ukweli mchungu kwa asilimia 100.Hongera sana kwa kuona hili.
 
Hii ni kuonesha kukubalika kwa cdm, na siyo tayari imeshinda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…