Mungu alipanga mwisho wa CCM kwa namna ambayo akili ya mwanadamu haiwezi kuelewa kirahisi. Aliamua aje mtu mgeni kwenye chama (Magufuli) ambaye atawanyang'anya chama wakongwe (Makamba, Kinana, Kikwete, Membe nk) na kuingiza watu wake wapya (Bashiru, Makonda, Polepole).
Hawa wapya kwa namna yake watakivuruga chama na misingi yake kwa maagizo yake Mafufuli. Wataleta chuki na maovu kama utekaji (Mo Dewji, Roma ) na uuaaji (Ben Sanane, Azory Gwanda nk).
Halafu watamshambulia mmoja wa viongozi wa upinzani (Lissu) kwa risasi za bunduki ya vita lakini mtu huyo hatokufa. Nchi nzima itashangaa namna mtu huyo alivyoshambuliwa, kunyimwa matibabu, kunyang'anywa mshahara kisha kufukuzwa ubunge.
Wanaposhangaa hayo na kumhurumia ndiyo watataka awe Rais wao wa 2020-25
Mungu ana sababu kwa kila jambo. Mwisho wa CCM ni mwaka huu. Alilopanga Mungu Binadamu hawezi kubadilisha. Hata kama NEC itaiba kura na kumtangaza Maguduli, nguvu ya umma itamtoa tu Ikulu. Wananchi wamechoka maonezi, dhuluma, ukandamizaji, ubaguzi na dharau