Video: Polisi watoa tamko baada ya kuzuiwa kupita kwenye barabara ya mwendokasi

Video: Polisi watoa tamko baada ya kuzuiwa kupita kwenye barabara ya mwendokasi

Mtemi mpambalioto

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2015
Posts
3,436
Reaction score
7,955

Kwa hiyo hata jengo la MWENDOKASI Likiwa linaungua hakuna kupitisha zimamoto humo wawahi kuzima?

Hawa ni walinda usalama wetu wanalinda mabenki, wanalinda wakuu wetu wa nchi, wanalinda hata ambavyo sisi kwa uelewa wetu hatuwezi ona! chukulia mfano kukawa na tukio hata la ujambazi ndani ya mwendokasi kituoni halafu hawa FFU wakawa karibu! najua watu wa mwendokasi watawakimbiloa polisi wawasaidie!

Mbona hizo mwendokasi zinapita tu barabara za Kimara mpaka Kibaha tena mwendo zaidi ya 50 na hawasimami kwenye Zebra ila polisi wanawachukulia poa tu?

What if walikiwa wanaenda kuzuia uhalifu?! Je, unaona unastahili kuongoza jiji hili?

Kwa hiyo mnataka AMBULANCE, MAJESHI YA ULINZI, POLISI, MADAKTARI wasipite mwendokasi wajae kwenye foleni huko?

msg-1440430540-188320.jpg


========================
Baada ya video inayoonesha askari Polisi wakizozana na walinzi wa barabara ya mwendokasi kusambaa mitandaoni, Jeshi la Polisi limetoa tamko kuwa hakuna aliyejuu ya Sheria.

Msemaji wa Jeshi la Polisi, SACP David Misime amesema wanatoa onyo kali na kuwa hakuna chombo chochote cha moto, baiskeli, mkokoteni au guta kupita katika barabara ya mwendo kasi.

Amesema bila kujali cheo cha mtu, yeyote atakayekaidi agizo hilo atachukuliwa hatua
 
Hii barabara inatumika pia kama emergency, chukulia ndugu yako amepandishwa kwenye ambulance na mnawahi labda Muhimbili mnazuiwa hivyo na anatumia oxgen au pili nyumba yako inaungua moto halafu zima moto wanazuiwa hivyo au hata pia wamepewa taarifa kuna mahali kuna panya road wanakuja halafu mnawazuia halafu kesho yake aliyejeruhiwa ni ndugu yako.

sio sawa.
 
Polisi wameshazoea kuishi maisha ya kujiamulia watakavyo..ata waliwa wanaenda kucheza mechi za ndondo cup watawasha ving'ora na kupita kwa kuforce kujionyesha wao ni miamba sana.
Huyo ni msimamizi wa usalama, hata kama alienda kucheza mpira kuna mtu alishika lindo, akimaliza anatakiwa awahi alipokuwa mahali pa kali mara moja na hii ni kwa sababu matatizo hayapigi hodi, police hana tofauti na ambulance au fire. akiwa on duty lazima awe eneo la kazi hata kama hakuna tatizo.
 
Kwa mtazamo wangu wenye zile special number deserve kupita popote including mwendo kasi - fire, ambulance, and police.

Wengine wanatakiwa kufuata taratibu hawako juu ya sheria au kwamba wao ni muhimu kuliko wananchi wengine.
 
Kwa mtazamo wangu wenye zile special number deserve kupita popote including mwendo kasi - fire, ambulance, and police.

Wengine wanatakiwa kufuata taratibu hawako juu ya sheria au kwamba wao ni muhimu kuliko wananchi wengine.
mimi mwenyewe ni mmoja wa wanaochukia police ila siku ukipata emergency kwako au kwa ndugu yako ndio watajua kwa umuhimu wa police, ambulance na fire kutumia hii lane.
 
Back
Top Bottom